Malkia Margreth II wa Denmark na mumewe, Henrik, wanatarajiwa kuwasili nchini Tanzania Novemba 3 kwa ziara ya siku nne kwa mwaliko wa Rais Jakaya Kikwete. Akizungumza na waandishi wa habari jana Jijini Dar es Salaam, Balozi wa Denmark nchini Tanzania, Bjarne Sorensen, alisema Malikia huyo na mumewe wanakuja na ujumbe wa watu 40 kutoka kampuni mbalimbali, wakiwamo wasanii 20. Sorensen alisema akiwa nchini Margreth II atafanya mazungumzo na Rais Kikwete kuhusu masuala mbalimbali kabla ya kwenda Zanzibar kuonana na Rais Amani Abeid Karume, kukagua miradi mbalimbali ya afya na kuangalia historia ya mambo ya kale visiwani humo. Sorensen alisema Malkia huyo na mumewe watakwenda Morogoro kutembelea Kijiji cha Dakawa, Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine na Wakala wa Mbegu za Miti Tanzania (TTSA)
No comments:
Post a Comment