.

.

.

.

Friday, November 14, 2008

MATANGAZO MAPYA YA UTALII TANZANIA YAZINDULIWA JIJINI LONDON

Waziri wa Utalii wa Tanzania Mh. Shamsa Mwangunga akikata utepe kuashilia uzinduzi rasmi wa London Tax 100 zitakazokuwa na matangazo ya Tanzania kwa miezi sita. Kilemba cha njano ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Utalii, Bi Blandina Nyoni. Sherehe hizo zilifanyika katika sehemu ya watalii ya London Eye.
Na Mwandishi Maalum
SERIKALI ya Tanzania imezindua kampeni kubwa ya matangazo ya utalii kwenye vituo vya treni ya chini ya ardhi na London tax nchini Uingereza yaligharimu Sh.milioni 800, yatatakayodumu kwa miezi sita.
Katika uzinduzi huo uliofanywa na Waziri wa Maliasili na Utalii, Shamsa Mwanguga, katikati ya jiji la London katika sehemu ya maarufu ya watalii ya "London Eye" iliyopo karibu na ukumbi wa bunge la Ungereza.
Waziri Mwangunga alikata utepe kwenye tax mbili zenye matangazo hayo zilizokuwa katika eneo hilo, kuashilia kuzinduliwa rasmi kwa tangaz hilo na baada ya hapo na ujumbe wake walikwenda katika kituo kikubwa cha treni cha Victoria kuangalia moja ya matangazo ya vituo vya treni.
Mkurugenzi wa kampuni ya Jambo Publications, Bw. Juma Pinto iliyoratibu matangazo hayo alisema Serikali imelipia matangazo 25 tu kwenye vituo vya treni, lakini imepata matangazo ya ziada kwenye vituo vitano zaidi na kufanya matangazo hayo makubwa kufikia 30.
Bw. Pinto alisema kampuni ya CBS inayoratibu matangazo hayo ya vituo vya treni imetoa matangazo mengine 15 kwenye vituo vya treni ya DLR na matangazo 1,000 ndani ya treni.Matangazo hayo yote yatadumu kwa miezi mitatu.
Mkurugenzi huyo wa Jambo alisema matangazo mengine yaliyopo kwenye mkataba huo ni London Tax 100 "Black Cab" na matangazo 200 yatakakuwa ndani ya hizo tax yametolewa bure.Matangazo hayo ya London Tax yatadumu kwa miezi sita na yanatarajiwa kumalizika mwezi Mei mwakani.
Awali mwaka mwaka huu mwezi Machi, Tanzania iliweka matangazo 100 kwenye mabasi ya London na matangazo sita katika uwanja wa ndege wa Heathrow, lakini baadhi ya watu wakidai kuwa hakuna matangazo yoyote yaliwekwa London.
"Mimi nadhani wanasiasa walikuwa wanataka kucheza mchezo wao mchafu kwenye haya matangazo, jambo ambalo haliingi akilini kusema kuwa hakuna matangazo wakati hadi leo kuna matangazo yetu pale Heathrow," alisema Bw. Pinto.
Alisema mwezi mMachi mwaka huu Serikali ililipia matangazo manne na tukaongezewe mawili na kuwa sita pale sehemu ya kuchukulia mizigo termian 4, matangazo yale yalikuwa yaishe mwezi Julai mwaka huu, hadi leo matangazo yapo na ndio yaliyoghalimu pesa nyingi.
"Haya matangazo ya Tanzania tunayafanya kwa umakini mkubwa kama daktari anaemfanyia mgonjwa operasheni, lakini kila siku panapokuwa na ukweli uongo unajitenga, sisi tunaendelea na kazi na watafute lingine," alisema Bw. Pinto.
Akizungumza katika uzinduzi kampeni hiyo, Waziri shamsa alisema Serikali ilishaweka bajeti yake ya matangazo tangu mwaka uliopita wa fedha na sasa kinachofanyika ni utekelezaji.
Waziri shamsa alisema awali Serikali ilizindua kampeni kama hii kule Marekani mapema mwezi uliopita kwenye televisheni ya CNN, hivyo awamu iliyobaki ilikuwa ni Ulaya na kuichagua Uingereza.matunda ya matangazo hayo yameanza kuonekana baada ya Marekani sasa kuongoza kupeleka watalii badala ya uingereza.
Alisema hivi sasa Tanzania imeamua kujitangaza na kuvitangaza vivutio vyake katika kuhakikisha tunapata watalii wengi zaidi ili tuweze kuongeza pato la Taifa na pia matangazo kama haya yanatumika kuitangaza nchi pia.
"Kweli tunaishukuru sana kampuni ya Jambo Publications kwa kutufanyia kazi hii, kweli imefanyika kama sisi tulivyotaka na tuna imani hata huko siku za baadae tutaendelea kufanya nao kazi na hata kama kulikuwa na matatizo kidogo basi ya kibinadamu tu, alisema Waziri Shamsa.
Alisema Serikali inakusudia kuongeza matangazo zaidi ya utalii kwa duniani kwa sababu imekuwa ikichangia sehemu kubwa ya pato la Taifa kutokana na watalii wengi sasa wanaongia nchini, hali inayofanya idadi yao kuongezeka mwaka hadi mwaka.
Alitoa tathmini ya watalii wa Uingereza wanaotembelea Tanzania alisema mwaka 1997 walifika watalii 25,000 hadi 2006 walifika 69,160 na mwaka 2007 idadi hiyo iliongezeka na kuamini idadi hiyo itaongeza mwaka huu.
"Tutashilikiana na balozi zetu kuhakikisha tunafanya juhudi kubwa za kuhakikisha tunafanikiwa katika kuutangaza utalii na kuna mikakati mingi tumeifanya na sasa ni utekelezaji wake unaendelea," alisema Blandina Nyoni.
Alisema sasa wanaelekeza nguvu kwa nchi za Ulaya na hapa Uingereza ndiyo sehemu muhimu hapa Ulaya, kwani ndiyo nchi ambayo inapokea wageni wengi kuliko nchi nyingine yoyote hapa Ulaya, hivyo kujitangaza hapa ni sawa na kujitangaza duniani.
Awali Balozi wa Tanzania Uingereza, Mwanaidi Senare Maajar alisema tayari ubalozi wake umekuwa ukifanya kazi kwa karibu na wizara ya utalii tangu mwaka jana.Balozi Maajar alisema Uingereza ni ufunguo muhimu katika sekta ya utalii wa Tanzania, hivyo wameweka mikakati mikubwa ya kufanyia kazi soko la utalii ili kuongeza idadi ya watalii na pia lengo la pili ni kuitangaza Tanzania.
"Tanzania tuna vivutio vingi sana ambavyo vinahitajika kutangazwa,na haya yaliyotangazwa katika matangazo ya sasa ni vichache tu kati ya vivutio vingi,serikali yetu inafuata misingi ya demokrasia na hata hali ya kisiasa ni nzuri na wananchi wake wana upendo mkubwa sana," alisema Balozi

No comments:

Post a Comment