Aisha Madinda amesema katika ‘intavyuu’ ya faragha iliyofanyika Sinza, Dar es Salaam kwamba watu hawajui ugonjwa unaomsumbua huku wengi wakipakaza mitaani kuwa tayari amekwishamkwaa mdudu.“Sina Ukimwi jamani, mimi nasumbuliwa na ugonjwa wa ajabu. Watu hawajui ninachoumwa. Kila nikifanya mapenzi hata mara moja, basi nitazidiwa na kulala kitandani wiki nzima,” alisema Aisha katika sura ya kuonesha kukata tamaa.Akiitolea ufafanuzi ‘ishu’ hiyo, Aisha alisema kuwa, mara nyingi huwa anazidiwa kila akikutana kimapenzi na mfanyabiashara mmoja mwenye jina kubwa jijini Dar es Salaam ambaye aliwahi kuwa mfadhili wa bendi nyingi nchini.Hata hivyo, Aisha aliomba kutotajwa gazetini kwa jina la kigogo huyo aliyepata kuwika sana kwenye muziki wa dansi nchini kwa madai kuwa ni mume wa mtu, hivyo ndoa yake inaweza kuharibika.“Ni huyo tu ndiye ananisumbua, nikifanya naye mapenzi nakuwa hoi, wiki nzima nalala kitandani ila nikitulia na kuwa mbali naye siumwi. Yaani nakuwa mzima kabisa,” alisema Aisha na kuongeza:“Imenibidi niyaseme haya kwa sababu yanayoenezwa mitaani ni mengi. Watu wananisingizia nina Ukimwi, jamani mimi siyo mgonjwa wa Ukimwi, nimekwishapima mara mbili na kukutwa salama kabisa.“Nasema hivi, kama kweli kuna watu wanaamini nimeathirika basi wamepotea, tena pengine wao ndiyo wagonjwa. Mimi ni mzima wa afya, ila tatizo ni hilo tu, nikikutana kimapenzi na huyo jamaa mambo yanaharibika.”Katika hilo, Aisha alisema kwamba kuna wakati huwa anaingiwa na hisia chafu kuwa amewekewa ‘tego’ la uchawi kwa huyo kigogo wa dansi na ndiyo maana kila akikutana naye kitandani, hubaki mgonjwa asiyetamanika.Aliendelea kuweka wazi ya kwamba kuna kipindi aliachana na mwanaume huyo na kuanzisha uhusiano na mtu mwingine ambaye walikaa naye kwa muda bila kusumbuliwa na maradhi yoyote, lakini aliporudiana na kigogo huyo wa dansi hadithi ya ugonjwa ilirudi ile ile.“Hapo utaona kwamba naumwa baada ya kufanya mapenzi na … (anataja jina la kigogo huyo wa dansi), lakini nikikutana na mwingine wala hata siumwi,” alisema Aisha.Alipoulizwa na mwandishi wetu kuwa anafikiriaje kuachana na mwanaume huyo kwa sababu ndiye chanzo cha matatizo yake, alijibu: “Unajua mimi na yeye tunapendana sana na ndiyo maana tunashindwa kuachana.“Fikiria kuwa kuna wakati tunaachana kabisa lakini kila tukikutana bila kutegemea tunajikuta kila mmoja anamtamani mwenzake, hivyo tunaamua kukumbushiana.”Hata hivyo, Aisha alisema kuwa hivi sasa atajitahidi kufanya juu chini mpaka aachane na mwanaume huyo kutokana na kile alichodai kuwa amekwishagundua kwamba yeye ndiye chanzo cha majanga yanayomkabili.Aidha, aliweka wazi ya kuwa sasa hivi anaye mchumba wake ambaye wana malengo ya kufunga ndoa, kwa hiyo atamsahau taratibu kigogo huyo wa dansi ili kujenga penzi lake jipya liwe imara.Kwa muda mrefu sasa, Aisha yupo kwenye mateso makubwa, akisumbuliwa na maradhi ambayo mpaka leo hayajawekwa wazi, licha ya kwamba kuna watu ambao ‘huchongoa’ midomo na kuutaja ugonjwa wa mnenguaji huyo mwenye jina kubwa, pasipo uhakika.Kutokana na maradhi hayo, muda mwingi Aisha amekuwa akiutumia hospitali na nyumbani kwake akijiuguza, huku kazini kwake, yaani kwenye majukwaa ya bendi yake ya African Stars International ‘Twanga Pepeta’ akionekana kwa mgao.
Source: GLOBAL PUBLISHERS
No comments:
Post a Comment