.

.

.

.

Monday, December 22, 2008

MANCHESTER UNITED MBELE KWA MBELE


Wachezaji wa Manchester United wakifurahia baada ya kuchukua ubingwa wa Kombe la Dunia - Vilabu huko Japan.
Huku wakicheza kumi uwanjani baada ya Nemanja Vidic kulamba kadi nyekundu Man U waliweza kufanya kile walichotazamiwa baada ya kuisambaratisha timu toka Ecuador Deportiva Universitaria Quito.
Man U ilionyesha kuutawala mchezo kipindi cha kwanza na kipindi cha Pili Equado walionyesha uhai na hata kukaribia kushinda hasa baada ya Vidic kutolewa lakini Rooney ndiye aliyekuwa nyota ya mchezo kwa kuwainua vitini mashabiki kwa kupachika bao la ushindi.

No comments:

Post a Comment