.

.

.

.

Monday, December 15, 2008

ROHO ZARUSHWA VILIVYO LONDON


Kundi la Jahazi Modern Taarab jana liliweza kukonga nyoyo za wapenzi wa muziki wa taarab Uingereza katika onesho lake lililofanyika katikaa ukumbi wa Silverspoon, uliopo pembeni ya uwanja wa mpira wa Wembley.Katika onesho hilo mahsusi kwa ajili ya sherehe ya miaka 47 ya Uhuru wa Tanzania lilihudhuliwa na Balozi wa Tanzania nchini Uingereza, Mwanaidi Sinare MaajarKundi hilo liliweza kuzikonga nyoyo za wapenzi wa muziki wa taarab kwa nyimbo kadhaa zikiwemo zilizopo kwenye albamu ya VIP, Two in one na nyinginezo zilizowafanya wapenzi kutotulia katika viti muda wote hadi mwisho wa onesho hili saa kumi alfajili..Kutokana na maombi ya wapenzi wa muziki huo hapa Uingereza, Jahazi watafanya maonesho mengine
Ijumaa ijayo tarehe 19/12/08 watakuwa katika ukumbi wa Lahore uliopo pembeni kidogo ya Job Centre,katikati ya mji wa Leicester.

Jumamosi taraehe 20 watakuwa Birmingham

Jumapili watawaaga wapenzi wao wa Uingereza katika onyesho lao la mwisho litakalofanyika Milton Keynes.








No comments:

Post a Comment