.

.

.

.

Tuesday, December 30, 2008

ZANZIBAR IMEMALIZWA KIUCHUMI NA BARA

Chama Cha Wafanyabiashara Wenye Viwanda na Wakulima Zanzibar (ZNCCIA) kimesema Zanzibar imemalizwa kiuchumi na Tanzania Bara na sasa wafanyabiashara wakubwa wanahamishia shughuli zao upande wa pili wa Muungano.
Akizungumza na waandishi wa habari Rais wa Chama hicho Abdallah Abass amesema kwamba sasa hivi kilichobakia kwa wazanzibari ni maneno matupu yasioonesha dalili kwa kufufuka kwa uchumi kwani biashara ndio imefikia kikomo chake.
Rais huyo alisema kwamba mikakati ya muda mrefu ya kuimaliza Zanzibar kibiashara imetimia kwani licha ya kuwepo kwa vikwazo visivyo vya kodi ndani ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mashaka mengine mapya yataikumba Zanzibar chini ya soko la pamoja la Afrika Mashariki.
"Tuliwahi kusema na tunaendelea kusema kuwa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imeshika bango kudumaza wafanyabiashara wa Zanzibar…tatizo la kulipishwa kodi mara mbili lipo pale pale, urasimu bado ni tatizo lakini pia wanachama wetu wanapata tatizo kupeleka biashara zao Tanzania bara wakati wenzetu wa bara wanaingiza bidhaa zao bila vikwazo," alisema Rais huyo.
Alisema kwamba matatizo mengine yanayochangia kuwakimbiza wafanyabiashara wa kizanzibari kuwekeza visiwani hapa ni kuwepo kwa taasisi nyingi zinazosimamia masuala ya kodi katika kisiwa kidogo kama Zanzibar na kuitolea mfano TRA na ZRB kuwa zinaongeza urasimu kwa wafanyabiashara

No comments:

Post a Comment