.

.

.

.

Sunday, January 25, 2009

CUF WALIA NA RAIS KIKWETE


KAULI ya Rais Jakaya Kikwete kuwa itawachukua muda mrefu wapinzani visiwani kuongoza dola, sasa imeonyesha wazi kupandisha hasira za wakazi wa Kisiwa cha Pemba na wanachama wa Chama cha Wananchi (CUF).
Habari zilizopatikana kutoka Kisiwa cha Pemba kinaeleza kuwa kutokana na kauli hiyo, baadhi ya wakazi wa kisiwa hicho wanaona kauli hiyo ya Kikwete ni ya kuwatangazia kuwakomoa kutokana na kutokipigia kura Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika chaguzi mbalimbali.
Wakizungumza na Mwananchi Jumapili kwa nyakati tofauti baadhi ya wananchi walisema hawakutegemea kama Rais Kikwete angetoa kauli hiyo hasa ikizingatiwa kwamba ndiye mtu pekee aliyekuwa kakitegemewa kunusu machafuko ya kisiasa Visiwani humo.
Katibu Mtendaji wa Wazee wa Kisiwa cha Pemba, Hamad Ali Musa alisema kauli za Rais Jakaya Kikwete ni za kinafiki na kwamba zimewapa nguvu katika hoja yao ya kuhakikisha kuwa kisiwa hicho kinapata utawala wake.
Mussa alisema jana kuwa wao walijua tangu awali kuwa CUF kinadanganywa na serikali ya CCM kuhusu mwafaka ndio maana wakaamua kuibua hoja ya kujitenga.
"Tangu awali tuliona CUF kinadanganywa na kuahadaliwa na serikali ya CCM na ndio maana tukaamua kuibua hoja ya kutaka kisiwa chetu kiwe na utawala wake," alisema Mussa na kuongeza;
"Pia tulijua kuwa serikali hii haiwezi kusimamia misingi ya demokrasia kwa kufanya mwafaka wa kweli na wa haki.
"Angalia sasa unafiki wa Rais Kikwete, huyu ndie mtu aliyekuwa akijinadi kuwa ana nia safi ya kushughulikia mpasuko wa kisiasa Zanzibar, je, leo anachokifanya ndicho alichoahidi bungeni?" alihoji.
Alifafanua kuwa Wazanzibari wamepoteza imani kwa Rais Kikwete kutokana na kutotekeleza kile alichowaahidi badala yake anazidi kuwatonesha na kufufua majonzi yaliyolala.
SOURCE- mwananchi

No comments:

Post a Comment