.

.

.

.

Sunday, January 25, 2009

HOFU YA VICHANGA YATANDA DAR-ES-SALAAM

Matukio mawili ya kutatanisha juu ya kuuawa kwa mtoto mchanga Jonathan Chale pale Mbezi Temboni Jijini na pia kutoweka kwa kichanga kingine kiutata wakati kikiwa mikononi mwa mama yake katika Hospitali ya Lugalo yamezua hofu ya aina yake kwa baadhi ya wakazi wa Jiji hili. Wakizungumza jana kwa nyakati tofauti, baadhi ya wakazi hao wamesema mazingira ya kutoweka kwa mtoto Jonathan, na kisha kubainika kuwa ameuawa kwa kunyongwa na kukatwa ulimi kabla ya kiwiliwili chake kufukiwa, yamewafanya wawe na shaka mpya juu ya usalama wa watoto wao. Wamesema vilevile kuwa hata mazingira ya kutoweka kwa mtoto aliyekuwa mikononi mwa mama yake pale katika Hospitali ya Lugalo yanazidisha hofu hiyo, ambayo jeshi la polisi Jijini kupitia kwa Kamanda wa Kanda yake Maalum ya Dar es Salaam, Kamishna Msaidizi Suleiman Kova, limesema liko kazini kuhakikisha kuwa hofu hiyo haipati nafasi. ``Haya matukio yanasikitisha na kuogopesha. Tunaambiwa mtoto alikuwa amelala ndani.... mara wakatokea watu, wakamuua kwa kumnyonga na kumkata ulimi kabla ya kumfukia ardhini. Wengine tunaanza kujawa na hofu kwa sababu tunaogopa mambo hayo yasije kuwakuta watoto wetu,`` akasema mkazi mmoja wa Manzese , aliyejitambulisha kama Mama Asia.

No comments:

Post a Comment