KAMBI ya Upinzani Bungeni imepanga kumbana Waziri Mkuu, Mizengo Pinda hadi ajiuzulu pamoja na serikali yake, baada ya kuwa na uthibitisho kuwa amevunja Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambayo aliapa kuwa atailinda wakati anapewa wadhifa huo.
Wapinzani hao hawakuishia hapo, pia wamemgeukia Rais Jakaya Kikwete wakimlaumu kuwa naye anafanya vitendo vya kuvunja umoja wa kitaifa pamoja na kwenda kinyume na mambo ambayo aliliahidi taifa wakati anaingia madarakani.
Akizungumza na waandishi wa habari mjini hapa, Msemaji wa Kambi ya Upinzani na Mbunge wa Wawi (CUF), Hamad Rashid Mohamed alisema kuwa wanamtaka Pinda kutoa maelezo ya kuliridhisha bunge juu ya wapi alipopata madaraka ya kwenda kinyume na katiba kwa kuwaagiza wananchi wajichukulie sheria mkononi kuwaua wale wanaowatuhumu kuhusika na mauaji ya watu wenye ulemavu wa ngozi (albino).
Alisema kuwa kambi ya upinzani ilikuwa na wasiwasi juu ya ukweli wa habari hiyo iliyotolewa kwa mara ya kwanza na gazeti hili, lakini jana walipata uthibitisho kutoka ofisi yake kuwa ni ya ukweli.
"Tumeshtushwa na hili kwani ni kinyume kabisa na misingi ya katiba yetu. Waziri Mkuu kuhamasisha wananchi kuchukua sheria mkononi, ni kitendo cha kulaaniwa," alisema Hamadi wakati akifafanua juu ya kauli hiyo aliyoitoa Pinda alipokuwa kwenye ziara Kanda ya Ziwa, hivi karibuni.
Mbunge wa Karatu (Chadema), Dk Wilbrod Slaa alisema hawakutarajia matamshi ya hatari namna hiyo yangeweza kutamkwa na kiongozi mkubwa serikalini.
Hata hivyo, alikataa kuweka wazi mikakati ambayo kambi hiyo ya upinzani itaitumia kufanikisha mpango huo kwa maelezo kwamba, ni sawa na askari wanaoenda vitani kuweka hadharani mbinu zao za
No comments:
Post a Comment