.

.

.

.

Friday, April 24, 2009

MENGI AMWAGA UPUPU



Mwenyekiti Mtendaji wa Makampuni ya IPP, Reginald Mengi, amewataja watu watano wanaotuhumiwa kuhusika na ufisadi mkubwa nchini na kuitaka serikali iwashughulikie haraka iwezekanavyo ili kuinusuru nchi kuyumbishwa nao. Watu hao, ambao Mengi alisema kwamba wanatuhumiwa kuwa ni `mafisadi papa`, ni pamoja na Mbunge wa Igunga na Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CC-CCM) na Halmashauri Kuu ya Chama hicho (NEC-CCM) Taifa, Rostam Aziz. Aliwataja wengine, kuwa ni wafanyabiashara, Tanil Somaiya, Yusuf Manji, Jeetu Patel na Subash Patel, ambao alisema wanatuhumiwa kuiba mabilioni ya wananchi na kuzihamishia nje ya nchi. ``Hawa wanatuhumiwa kuiba mabilioni ya fedha za wananchi, na baya zaidi fedha hizo zimehamishiwa nje ya nchi,`` alisema Mengi alipozungumza na waandishi wa habari katika Ofisi za IPP Limited, jijini Dar es Salaam jana na kuongeza: ``…mafisadi wote na hasa wale wanaotuhumiwa kuwa mafisadi papa ni lazima washughulikiwe, la sivyo wataiyumbisha na kuitingisha nchi yetu. Ni lazima Watanzania tuone kwamba sasa tumefika mahali pa kusema imetosha.``

No comments:

Post a Comment