Mwenyekiti wa TLP Tanzania Labour Party Augustin Lyatonga Mrema, ameonywa na mpinzani wake anayegombea nafasi ya Uenyekiti Taifa kwa kupitia chama hicho, Bw Mtumgerehi wakati wa Mkutano mkuu wa chama hicho uliofanyika katika hoteli ya Starlight jijini. Bw. Benardicto Mtungurehi aliwaambai waandishi wa habari kuwa Mrema kwa sasa hana jipya kwanza anafuja mali za chama ambapo kwa mwezi anachukua pesa za ruzuku shilingi milioni 7 je muulizeni anazipeleka wapi . Pia anatumia mali za chama kama mali yake kwa mfano anaishi katika nyumba ya TLP na anatumia Gari la chama mbona hivyo hasemi, kwahiyo sisi wanachama tunataka kujua pesa zote hizo zinakwenda wapi. Aliendelea kuwauliza waandishi hebu jifikirie leo ni Mkutano wa wanachama wa Halmashauri Kuu, sasa iweje ageuze kama mkutano wake mumeona wenyewe akisoma hutuba yake ambayo hapa si mahala pake. Sisi tunasema lazima aondoke kwa vyovyote vile tumeshamchoka.
No comments:
Post a Comment