Simba na Yanga ( MAREKANI) zitapambana Jumapili ya April 26 ikiwa ni moja ya sherehe za muungano,homa imezidi kupanda miongoni mwa wachezaji na washabiki wakitambiana kila mmoja akivutia kwake,hii imetokana na mechi ya Simba na Yanga (TANZANIA)) kutoka 2-2,kila timu ikisema imetumwa kumalizia kazi iliyokua imebakizwa Simba/Yanga Tanzania.
Kambi za timu zote ni shwari isipokua Yanga golikipa Dedy Luba ameumia mkono baada ya kungongana na Kheri Kheri kwenye mazoezi,kocha wa Yanga Meya ameingiwa na wasiwasi wa kumkosa kipa huyo,kwa upande wa wachezaji wengine amesema wapo fiti na wanaendelea vizuri na mazoezi na atatangaza kikosi ijumaa.
Kambi ya Simba inaendelea vizuri chini ya kocha mchezaji Libe,na wamemrudisha kipa Hiraly aliyekua ameihama timu kwa kisingizio cha kua benchi muda mrefu na habari ndani ya kambi hiyo zina sema huenda wakamrudisha Londa ambaye kwa sasa yupo Tanzania kwa Shughuli za kifamilia lakini Mkakile(Bamchawi) alipoulizwa alikataa kuthibitisha habari hizi kwa kusema haya ni mambo ya ndani ya uongozi wa Simba,wakati huo huo Yule mchezaji wa kiungo wa Simba ambae kwa sasa yupo Atlanta Elvis Dotto Mnyamuru atakuja maalum kwa mechi hio jumapili.
Kocha mchezaji wa Simba alipoulizwa kikosi gani kitashuka dimbani,alisema sasa hivi ni mapema kutangaza kikosi kwani wacheaji wote wapo kwenye ari na mazoezi yamepamba moto,lazima tuigalagaze Yanga mwaka huu. Mgeni wa heshima kwenye mechi hii atakua msaidizi balozi mh Switebert Mkama,mechi itachezewa kwenye wanja letu la Taifa la zamani (Meadowbrook park),saa kumi na moja jioni(5:00pm) pia Nyama choma itakuwepo,washabiki manaombwa kuja kwa wingi na kuwa wa tulivu mechi itakua nzuri na burudani tosha kuadhimisha SIKU YA MUUNGANO.
No comments:
Post a Comment