.

.

.

.

Monday, May 18, 2009

SHOGA ALETA KIZAIZAI MWANANYAMALA HOSPITALI

UMATI ulifurika jana katika hospitali ya Mwananyamala, mjini Dar es Salaam kumwona mgonjwa aliyefikishwa hospitalini hapo anayesadikiwa kubadili jinsia kutoka ya kiume kuwa ya kike. Kwa mujibu wa vyanzo vya habari ndani ya hospitali hiyo, mgonjwa huyo alifikishwa hapo saa 11.00 alfajiri ya jana akiwa hajitambui, baada ya kuokotwa na polisi maeneo ya Mbezi Beach. Chanzo cha habari kilisema iliwawia vigumu wauguzi kutokana na mgonjwa huyo, ambaye kimtazamo anaonekana mwanaume lakini alitambulishwa kwa jina la mwanamke. "Alipokaguliwa alikuwa na jinsia ya kike iliyoonekana ni ya bandia, aliyowekewa kwa njia ya operesheni kwa sababu kuna mishono ya nyuzi kwenye sehemu za siri,Ó kilidai chanzo hicho cha habari na kuongeza kuwa alikuwa amevaa hereni. Kwa mujibu wa chanzo cha habari, baada ya ukaguzi huo, mgonjwa huyo alipelekwa wodi namba tatu ambayo ni ya wanawake. Mganga Mkuu wa Hospitali ya Mwananyamala, Dk. Suleiman Mtani, akizungumza na Uhuru hospitalini hapo alikiri mgonjwa huyo kulazwa katika wodi ya kinamama. Alisema kimaadili kazi yao ni kuhudumia wagonjwa bila kujali jinsia wala historia ya maisha yao. "Ni kweli tuna mgonjwa wa aina hiyo aliyeletwa na polisi alfajiri ya leo lakini hatuwezi kuwaruhusu mkamwone kwa kuwa hajielewi na kimaadili kazi yetu ni kumtibu mgonjwa apone na aendelee na shughuli zake, hatujali alikuwa jambazi, shoga au mwizi, sisi tunatibu mengine ni yake," alisema Dk. Mtani. Aliongeza: "Kwa sasa hajielewi sisi ndio tunatunza siri zake mpaka apate fahamu na kama mtataka kuzungumza naye kwa ridhaa yake akikubali mtazungumza naye lakini leo hatutawaruhusu. ÒKwa kuwa huyu aliletwa na polisi ili atibiwe ni vyema mkaulize habari zake polisi watawaeleza ni wapi walimkuta na mazingira waliyomkutaÉ watawapeni maelezo kamili". Kutokana na hilo, uongozi wa hospitali ulilazimika kubandika tangazo kuzuia watu kuingia ndani ya wodi hiyo. Kamanda wa Polisi Wilaya ya Kawe, Hendry Mwaibambe, alisema kwa mujibu wa taarifa walizonazo mtu huyo anadaiwa kuwa shoga. Alisema jana alfajiri aliokotwa eneo la Mbezi Beach akiwa hana fahamu na kuamua kumpeleka Mwananyamala ili akatibiwe. Kwa mujibu wa Mwaibambe, shoga huyo (jina linahifadhiwa) ni mkazi wa Kawe, ambaye aliuza nyumba yake ili akabadilishe jinsia nchini Thailand, ili apate soko ambalo hakupata. Kamanda Mwaibambe alisema kutokana na hilo, alichanganyikiwa na inasadikiwa alikunywa sumu ili ajiue.

No comments:

Post a Comment