.

.

.

.

Wednesday, June 10, 2009

BUKWIMBA ALA KIAPO

Mbunge mteule wa Jimbo la Busanda (CCM), Lolesia Bukwimba, amepishwa ndani ya ukumbi wa bunge muda mfupi uliopita huku kambi ya Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) ikipuuza vikali uapishaji huo na kudai hawautambui.Wakati hayo yakitokea wabunge wa CCM walimsindikiza ndani ya ukumbi wa bunge, wakiimba: “ CCM,…CCM..CCM.”Katika msafara huo ambao mbunge mwanaume alikuwa ni William Ngeleja pekee, wabunge hao waliendeleza shamrashamra hizo hadi karibu na eneo la kiapo ndipo wakarejea katika viti vyao.Wakiwa katika viti vyao, baada ya Bukwimba kula kiapo, vilisikika vigelegele, nderemo na vifijo. Nderemo hizo na vifijo, vilisikika huku kukiwa na maneno ya chini kwa chini ambapo sauti ya Waziri wa Nchi (Ofisi ya Rais Utawala Bora) Sophia Simba, ilisikika akichomekea maneno kama: “Habari ndiyo hiyo…”“Chadema wako wapi, wameingia mitini… Chadema mpo?…”

No comments:

Post a Comment