Kuna dalili kubwa za serikali kuutwaa mgodi wa Mawe Kiwira kutoka mikononi mwa wawekezaji ambao Kampuni ya Tanpower Resources Ltd ambayo inamilikiwa na familia ya Rais mstaafu, Benjamin Mkapa na aliyekuwa Waziri wa Nishati na Madini, Daniel Yona.
Waziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja, alisema taarifa ya hatua zitakazochukuliwa dhidi ya mgodi huo ataitoa bungeni na kwamba, serikali imeamua kukwamua mradi huo.
Taarifa ambazo zilipatikana kutoka ndani ya Kamati ya Bunge ya Nishati na Madini, zilidai kuwa miongoni mwa mapendekezo iliyopeleka serikalini ni kuchukua mradi huo kwa sababu, mwekezaji ameshindwa.
Pia, kamati hiyo ilitaka kujua sababu zilizosababisha fedha zilizotolewa na serikali kwa mwekezaji hazikufanya kazi iliyokusudiwa.
Tanpower Resources Ltd, inayomilikiwa kwa pamoja na familia ya Mkapa na Yona, ilimilikishwa mgodi huo na ulikuwa umepangwa kukamilika mwaka huu, lakini umekwama na hadi sasa wafanyakazi wanadai mamilioni ya fedha kama malimbikizo ya mishahara. Akizungumza na wahariri wa vyombo vya habari jana, Ngeleja alisema serikali imeamua kukwamua uendelezaji wa mradi huo awamu ya kwanza ya kuzalisha umeme wa megawati 200.

No comments:
Post a Comment