.
.
Tuesday, June 09, 2009
WAFIA HOTELINI DSM
WATU wawili wenye asili ya kiasia wamekutwa wamefariki dunia katika hoteli ya Harbour View Suit, mjini Dar es Salaam. Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi Suleiman Kova, alithibitisha kutokea kwa tukio hilo ambapo aliwataja marehemu kuwa ni Salman Zubeir (41) raia wa Canada na Yusuph Sader (33), raia wa Afrika Kusini. Akieleza mazingira ya vifo hivyo, Kova alisema vilitoke juzi mchana na kwamba marehemu hao walikunywa pombe kali zinazohisiwa huenda ndizo zilizosababisha vifo vyao. "Siku ya tukio walionekana wakinywa hotelini hapo na baadaye kuhamia Club Bilcanas, ambako walikunywa hadi asubuhi waliporudi hotelini kulala na baadaye kugundiliwa wamekufa," alisema Kamanda Kova. Kwa mujibu wa Kova, Meneja Mauzo wa hoteli hiyo, Leza Mnukwa (51), ndiye aliyemgundua marehemu Zubeir aliyekuwa chumba namba 1011 baadaye rafiki wa marehemu Sader, Nikhil Twalwar (33), naye aligundua rafiki yake huyo amefariki dunia. Mnukwa na Talwar wanashikiliwa na polisi kwa uchunguzi zaidi huku maiti za marehemu hao zikiwa zimehifadhiwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili. Kova alisema uchunguzi wa vifo hivyo unaendelea na kuwa wamechukua matapishi yaliyopatikana vyumbani mwa marehemu hao kwa uchunguzi utakaomhusisha Mkemia Mkuu wa Serikali na daktari maalumu kutoka jeshi la polisi. Marehemu hao ambao walikuwa wanafahamiana waliingi nchini tangu Mei 19 kibiashara na walipanga na kuishi hotelini hapo hadi vifo vilipowakuta. Wakati huohuo, kundi kubwa la wanafunzi wanaoishi hosteli za Mabibo, juzi usiku liliyatupia mawe magari yaliyokuwa yakipita katika eneo la Extenal barabara ya Mandela na kufanikiwa kuharibu moja aina ya Toyota DCM ambalo namba zake hazikuweza kupatikana, kushinikiza kuwekwa matuta kutokana na kugongwa kwa wenzao wawili. Aliwataja wanafunzi waliogongwa na pikipiki, kuwa ni Ibrahimu Mkama (25) na Sayuni Daniel (30) ambao walipata majeraha madogo waliyotibiwa katika kituo cha afya kilichopo katika hosteli hizo na kuruhusiwa. Kutokana na tukio hilo, alisema kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa itatoa tamko kuhusu hatua zinazoweza kuchukuliwa kwa waliohusika kwenye tukio hilo.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
can anyone translate this news in English please!
ReplyDeletehttp://www.dailynews.co.tz/home/?n=2424
ReplyDelete