.

.

.

.

Wednesday, October 14, 2009

KANDA YA ZIWA YAZIDI KUTESA KWENYE MASHINDANO YA BURUDANI

Kanda ya Ziwa imeendelea kutesa katika anga ya burudani ambapo juzi usiku mshiriki wa shindano la kusaka vipaji la waimbaji (Bongo Star Search) kutoka Mwanza, Pascal Cassian aliibuka kidedea katika shindano hilo. Ikiwa ni siku ya 12 baada ya kumalizika kwa kinyang’anyiro cha kumsaka mnyange wa Tanzania (Vodacom Miss Tanzania 2009), kutoka Mwanza Miriam Gerald kung’ara katika mshikeshike huo imeweza kuiwekea historia mkoa huo kutoa washindi mfululizo ndani ya mwaka huu.

Kutokana na ushindi huo Miriam aliyetwaa taji hilo na kunyakua zawadi zenye thamani y ash mil. 61 ikiwa ni gari ya thamani ya mil.53 pamoja na fedha taslim sh mil.9. Aidha kutokana na ushindi huo Cassian amezawadiwa mfano wa hundi ya fedha yenye thamani kiasi cha sh.mil. 25 toka kwa wadhamini wakuu wa fainali hizo Vodacom Tanzania. Nafasi ya pili ilikwenda kwa mshiriki kutoka Kigoma Peter Msechu ambaye amepata zawadi y a sh mil.5, mshindi wa tatu ni Kelvin Mbati aliyepata kitita cha sh mil3.5. Huku katika hatua nyingine mshiriki kutoka Tanga Jackson George aliyepata sh mil.1.5 na wa tano ni Beatrice William aliyepata sh mil 1,huku washiriki waliofanikiwa kuingia kumi bora kila mmoja akiibuka na sh.400,000. Mbali na Vodacom, BSS mwaka 2009 imedhaminiwa pia na kampuni ya bia Tanzania (TBL) kupitia bia ya Kilimanjaro, Family Health International, Tansoma Hotel na Maji ya Kilimanjaro.

No comments:

Post a Comment