Mke wa Rais Mama Salma Kikwete ametunukiwa tuzo ya Mama wa upendo na wanafunzi wa shule za Sekondari za Mvomero mkoani morogoro ikiwa ni ishara ya shukrani za wanafunzi hao kwa jinsi anavyowajali na kuwasaidia watoto wenye shida.
kufundishia, kuweka matanki ya maji na kufunga umeme wa jua katika
Mama Kikwete alikabidhiwa tuzo hiyo jana na Mariam Kaima ambaye ni mwanafunzi wa kidato cha tano katika shule ya sekondari ya Adrian Mkoba kwa niaba ya wanafunzi wenzake wakati wa tamasha la wanafunzi wa shule za Sekondari wa wilaya ya hiyo lililofanyika katika ukumbi wa mikutano wa chuo kikuu cha Mzumbe.
Akitoa shukrani kwa niaba ya wenzake Mariamu alisema kuwa Mama Kikwete ni mama na kiongozi wa kwanza hapa Tanzania kuhimiza watu wote kuwapenda watoto wa wenzao kama wanavyowapenda watoto wao, kuwasomesha watoto zaidi ya 300 ambao ni yatima na wanaoishi katika mazingira hatarishi, kutoa misaada ya vifaa vya shule za Sekondari.
Aidha Mama Kikwete kupitia Taasi yake ya Wanawake na Maendeleo (WAMA) inatoa misaada ya vifaa vya afya ili kupunguza vifo vya wanawake wajawazito na watoto, kuendeleza kampeni za kutokomeza mimba za utotoni na kutumia muda mwingi wa kuzungumza na wanafunzi juu ya changamoto zinazowakabili.
Wanafunzi hao walimuahidi Mwenyekiti huyo wa WAMA kuwa watakemea utoro na kuwafichua watoro wote, kuwaumbua hadharani mafataki wote wanaowasumbua watoto wa kike, kupinga mimba za utotoni, kuepuka mimba za utoto kwa kuepuka kufanya mapenzi katika umri mdogo na kuongeza juhudi katika masomo ili kuongeza kiwango cha ufauliu.
Kwa upande wake Mama Kikwete aliwashukuru wanafunzi hao kwa kuona umuhimu wa kazi anazozifanya kupitia Taasisi yake ya WAMA na kuwataka kukazana katika masomo yao ili weweze kupata elimu ya kutosha itakayowasaidia maishani mwao.
"Nafasi ya kusoma mliyoipatamuitumie kwa kusoma kwa bidii na kuwa na maendeleo mazuri kitaaluma ili wale wanaowasomesha wapate moyo wa kuwasomesha zaidi kwani kuna wenzenu wanatafuta nafasi kama hii lakini haipati", alisema Mama Kikwete.
No comments:
Post a Comment