.

.

.

.

Monday, October 26, 2009

MTOTO WA AJABU

Mtoto Ali Yakubov mwenye umri wa miezi tisa amepata umaarufu mkubwa na amekuwa gumzo dunia nzima baada ya taarifa za miujiza yake ambapo maneno tofauti tofauti ya kiarabu kuanza kutokea kwenye mwili wake.

Maandishi ya kiarabu yanayonukuu aya za Quran yamekuwa yakitokea kwenye mikono yake, miguu na tumboni na kisha kutoweka baada ya siku kadhaa na kisha maandishi mengine ya kiarabu yanayonukuu vipande tofauti vya aya za Quran hujitokeza upya.Madaktari nchini Urusi hadi leo bado hawajui nini kinaendelea kwenye mwili wa mtoto huyo ambaye maandishi ya kwanza ya kiarabu yanayosema neno "Allah" yalijitokeza kwenye kidevu chake ndani ya wiki moja baada ya kuzaliwa.

Awali watu wanaopinga miujiza ya mtoto huyo walianza kuvumisha kuwa wazazi wa mtoto huyo ndio wanaomuandika maneno hayo mtoto huyo lakini madaktari wamepinga uvumi huo na kusema kwamba maandishi hayo si maandishi ya mtu kuandika juu ya ngozi kwani yanatokea toka ndani ya ngozi ya mtoto huyo.Mama wa mtoto huyo, Madina alisema kwamba yeye na mumewe walikuwa si watu wa dini mpaka maandishi hayo yalipoanza kutokea.Awali maandishi hayo yalipotokea hawakutaka kumuonyesha mtu yoyote mpaka walipomuonyesha daktari wao na baadae imamu wa mji wao kuitwa kuangalia maandishi hayo.Hivi sasa mtoto huyo ameufanya mji wa Dagestan, kusini mwa Urusi uwe maarufu sana kwani mamia ya watu kutoka kona mbali mbali duniani wanamiminika kwenye mji huo kumuona na kuomba dua mbele ya mtoto huyo."Huyu mtoto ni dalili tosha ya kuwepo kwa Mungu", alisema mbunge wa mji huo Akhmedpasha Amiralaev na kuongeza "Mungu amemleta Dagestan ili kusaidia kuiokoa jamii yetu".

Mama wa mtoto huyo alisema kwamba kawaida maandishi hayo hutokea mara mbili katika kila wiki, siku ya jumatatu na usiku wa kuamkia ijumaa."Ali husikia maumivu makali wakati maandishi haya yanapoanza kujitokeza, hulia sana na joto la mwili wake huwa juu sana, ni vigumu kumshikilia wakati maandishi hayo yanapokuwa yakitokea kwahiyo huwa tunamuacha kwenye kiti chake", alisema mama wa mtoto huyo.Mama huyo aliendelea kusema kuwa aya tofauti hujitokeza kila maandishi mapya yanapotokea.Imamu wa mji huo Imamu Abdullah amekuwa akiwaambia watu wanaoshangazwa na mtoto huyo kwamba Quran ilishatabiri kuwa kabla ya kiama watatokea watu wenye maandishi ya quran kwenye miili yao.Mojawapo ya maandishi yaliyojitokeza kwenye mwili wa mtoto huyo ni yale yanayosema "Usizifiche dalili hizi kwa watu".

No comments:

Post a Comment