Pichani: mustafa akipozi na stella na adil wa kampuni ya infinity ambayo inafadhili Swahili Fashion week.
Kwa mara ya pili mfululizo wiki ya mitindo –Swahili Fashion Week (SFW) - itafanyika tena jijini Dar Es Salaam na kuwapa wapenda mitindo siku tatu zilizojaa shoo za mitindo za aina mbali mbali.Swahili Fashion week ni siku chache za mitindo ya kisasa yenye mahadhi ya uswahili na vile vile hujumuisha wabunifu wa mavazi wenye vipaji kutoka sehemu mbali mbali nchini, nchi zinazozungumza Kiswahili na nchi nyinginezo. Katika onyesho hilo wabunifu huonyesha kazi za kipekee zenye mahadhi ya kiafrika zikijumuisha, nguo, viatu, mapochi na urembo mwengine.Akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa onyesho hilo la mavazi mwanzilishi wa SFW Mustafa Hassanali ambaye ni mmoja wa wabunifu maarufu nchini alisema mwaka huu Swahili Fashion Week inahamasisha ‘Mitindo kama biashara.’“Swahili Fashion Week mwaka huu ni mwanzo wa ari mpya; tunaandaa onyesho litakalohamasisha mitindo kama biashara. Tunataka kukuza shughuli za mitindo nchini ili isiwe inachukuliwa kama fani ya burudani bali mojawapo ya njia za kukuza kipato.Ulimwenguni kote fani ya mitindo ni moja kati ya fani zinazochangia katika uchumi wa nchi, hivyo basi na sisi tungependa kusisitiza umuhimu wa fani hii nchini ili watu waipe umuhimu unaotakiwa kama njia mojawapo ya kuongeza ajira na kuondoa umaskini kwa ujumla,” alielezea Hassanali.Wiki ya Mitindo ya mwaka huu itajumuisha wabunifu mavazi 14 kutoka mikoa mbali mbali nchini na wabunifu 6 kutoka nje ya nchi na maonyesho hayo ya mavazi yatafanyika tarehe 4 hadi 6 novemba mwaka huu katika viwanja vya Karimjee jijini Dar Es Salaam.“Swahili Fashion week inatoa nafasi kwa wabunifu wanaoibuka na waliobobea kuonyesha kazi zao ndani ya paa moja na hivyo kuwapatia nafasi wabunifu wakongwe kuwapa ushauri wale wachanga.British Council inashiriki katika hili kwa kuaanda tuzo ya mbunifu asiyejulikana mwenye kipaji inayoitwa ‘Emerging Designer Award.’ SFW pia inatoa nafasi ya kipekee kwa wabunifu kukutana pamoja kubadilishana mawazo na pia kupata ujuzi zaidi kupitia warsha mbali mbali zitakazoandaliwa na Goethe Institute,” aliongeza Hassanali.Kama ilivyokuwa SFW ya 2008, mwaka huu pia washiriki wa fainali za shindano la kisura wa Afrika maarufu kama ‘M-net Face of Africa’ watashiriki katika maonyesho hayo ya mitindo kama sehemu ya shindani hilo kwa kuonyesha mavazi.Wabunifu wanaoshiriki katika SFW wanachaguliwa na bodi ya wana mitindo inayoitwa ‘Fashion Advisory Board (FAB)’ ambayo wajumbe wake ni pamoja na Emelda Mwamanga Mkurugenzi Mkuu wa Jarida la Bang, Mwanasheria Matukio Chuma, Mkurugenzi wa sanaa na promosheni wa BASATA Nsia Shalua, na mmiliki wa klabu maarufu ya starehe jijini Dar es Salaam Abigail Plaatjees.Maonyesho ya Swahili Fashion Week mwaka huu yanaletwa kwa ushirikiano na kampuni za Vodacom Tanzania na ZTE.Vile vile wadhamini wngine ni, Infinity Communications Ltd, REDDS, Southern Sun, Goethe Institute, British Council na BASATA.Pia wadhamini wengine ni Ultimate Security, Primetime Promotions, Vayle Springs, ZG Designs & Films, Jan Malan Umzingeli, Choice Fm & Clouds fm, Mwananchi Communications Ltd, Brooklyn Media, 1&1 Internet solutions, Channel Ten, Imaging Smart, IMAN Cosmetics, Darling, Runway Lounge, Perfect Machinery na African Life Assuarance.
No comments:
Post a Comment