Rais JAKAYA KIKWETE akielekea kukagua gwaride la heshima lililoandaliwa na vikosi vya Jeshi la Ulinzi la Wananchi JWTZ leo kwenye uwanja wa Uhuru mara baada ya kuapishwa kushika madaraka kama Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa miaka mingine mitano kufuatia ushindi wake alioupata dhidi ya wapinzania wake katika uchaguzi mkuu uliofanyika wiki iliyopita nchini kote.
Rais Robert Mugabe wa Zimbabwe alikuwepo katika Sherehe za kuapishwa kwa rais Jakaya Mrisho Kikwete leo hapa anaonekana akiingia kwenye gari.
Rais Mwai Kibaki wa Kenya Kulia pamoja naye .Prof. George Saitoti Waziri wa Usalama wa Mambo ya Ndani Kenya wakiwa tayari kwa kuondoka kwenye uwanja wa Uhuru leo
Rais Jacob Zuma wa Afrika Kusini akisindikizwa na waziri wa Mwenyekiti wa UWT na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Utawala Bora Sofia Simba akimsindikiza wakati rais huyo alipokuwa akiondoka uwanjani hapo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Dk Mohamed Gharib Bilal akielekea kwenye gari ili kuondoka uwanjani hapo lmara baada ya kula kiapo leo.
No comments:
Post a Comment