.

.

.

.

Saturday, December 18, 2010

NOTI MPYA ZATOLEWA NA BENKI KUU TZ

Benki Kuu ya Tanzania leo imetangaza kutoa toleo jipya la noti ya sh 500,1000,2000, 5000 na 10000. Noti hizo zitaingia katika mzunguko Januari Mosi mwakani na zitaenda sambamba na noti zilizopo sasa.
Gavana wa Benki hiyo Prof.Benno Ndullu amesema wakati akizindua noti hizo kwamba noti za zamani zitaendelea kutumika mpaka zitakapomalizika zenyewe katika mzunguko na
wananchi wazipokee na kuzitumia.
Amesema pia hakutakuwapo na ubadilishaji wa kupeleka noti za zamani benki na kutaka kupewa noti mpya.Katika maelezo yake amesema kwamba toleo hilo jipya lina taswira inayozingatia maendeleo ya uchumi na Jamii ya Tanzania.
Alisema kuna ambadiliko kidogo katika toleo jipya ambapo waasisi wa taifa hili, Mwalimu Julius Nyerere na Sheikh Abeid Amani karume wamewekwa katika toleo jipya.Nyerere anaonekana katika noti ya shilingi elfu moja na Karume katika noti ya sh 500. Noti tatu zilizosalia yaani elfu mbili, tano na kumi zitaendelea kuwa na picha za wanyama pori ambao wanapatikana kwa wingi kwenye hifadhi na mbuga zetu za wanyama.
Hata hivyo kutokana na kupungua kwa ukubwa wa noti wameweka vichwa wanyama badala ya wanyama wazima kama ilivyo katika noti za zamani.
katika kupambana na wale wanaotengeneza noti bandia na kuongeza uhai wa fedha hizi katika mzunguko kabla ya kuchakaa toleo jipya limeongezwa ubora kw akuwekwa alama maalumu mpya za usalama na kutumia taaluma mpya kuziimarisha.
kwa mara ya kwanza kumewekwa pia alama nyingine ya usalama alama ya motion ambayo ni rahisi sana kutambulika kwa macho.
gavana amewataka wananchi kufuata maelekezo ya alama z ausalama za noti hizo na kwamba wataendelea kutoa elimu na pia watuw anaweza kufuatia taarifa hizo katika mtandao wa kompyuta:www.bot-tz.org

No comments:

Post a Comment