Mhe. Balozi Radhia Msuya, Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Afrika Kusini, akiwasha Mwenge, ikiwa ni ishara ya kuadhimisha Sherehe za Kitaifa za Kutimiza Miaka Mia Moja ya kuanzishwa kwa Chama Cha ANC cha Afrika Kusini.
Sherehe hizo zilianza katika vitongoji na miji kadhaa nchini Afrika Kusini tangu mwezi Januari 2012, ambapo viongozi mbalimbali wa Kitaifa walihudhuria, wakiwemo Mhe. Rais Jacob Zuma ambaye alikuwa mgeni rasmi, Rais mstaafu Mhe. Benjamin W. Mkapa, pamoja na marais na viongozi wa nchi mbali mbali.
Mjumbe wa Chama cha ANC, Bw. Sochayile Khanyile, naye akiongea machache wakati wa Sherehe hizo.
Mhe. Balozi Radhia Msuya, Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Afrika Kusini akisema machache wakati wa Sherehe za Mwenge za kuadhimisha Miaka 100 ya Chama Cha African National Congress (ANC) zilizofanyika hivi karibuni tarehe 30 Oktoba, 2012 kwenye Ofisi za Ubalozi wa Tanzania mjini Pretoria, Afrika Kusini.
No comments:
Post a Comment