.

.

.

.

Sunday, December 09, 2012

KLABU MPYA YAZINDULIWA MIKOCHENI D'SALAAM



Wapenda burudani wa jiji la Dar es Salaam mwishoni mwa wiki hii wamesherekea uzinduzi wa Club mpya inayojulikana kama 327, iliyopo mitaa ya Mikocheni katika usiku uliopambwa na burudani na vinywaji.

Wageni waalikwa waliachwa midomo wazi na namna klabu hiyo ilivyopambwa, sehemu pana ya bar, muziki mzuri pamoja na vyumba vitatu vya wageni maalumu vilivyobuniwa na kupambwa na Moet-Hennessy.

Kabla ya uzinduzi rasmi wa club hiyo ulioanza saa tano kamili usiku, kulitanguliwa na sherehe maalumu iliyohudhuriwa na wageni 125 waliokaribishwa na Moet na Chandon. Wageni hao waalikwa walitembezwa ndani ya club hiyo yenye ghorofa mbili pamoja na vyumba vya wageni maalumu vya Moet na Chandon, Hennessy pamoja na Belvedere. Mmiliki wa club hiyo, bwana Lawrence Kadri aliwashukuru wageni waalikwa kwa hotuba fupi iliyofuatiwa na ufunguaji wa shampeni ya Moet na Chandon.


Wageni waalikwa pia walipata burudani kutoka kwa mburudishaji kutoka Kenya, Miaia Van Lekow.
Baada ya sherehe kufunguliwa rasmi saa tano kamili usiku, club 327 ilipamba moto kwa sherehe kuanza rasmi ikiwajumuisha watu wote maarufu hadi ilipokaribia nyakati za asubuhi.
Akizungumza wakati wa uzinduzi, Kadri alisema amefurahishwa na mapokezi makubwa ambayo club yake imepata, akiwahakikishia kuwa club hiyo itakuwa sehemu nzuri ya mapumziko lakini kwa gharama nafuu zaidi. ‘Club hii inatofautiana na club nyingi hapa mjini sio tu kwa namna ilivyopambwa bali kwa bei zetu nafuu pia, kwani tunafikiri wageni wetu wana haki ya kufurahia huduma zetu bila kutoboa mifuko yao’ alisema Kadri.

Uzinduzi wa Club hii umekuja kama habari nzuri kwa wapenda burudani wengi hasa watu wa kipato cha kati ambao mara nyingi wamejikuta wakiishia kwenye baa za mitaani kama mbadala wa sehemu nzuri zenye bei kubwa. Hakika kitu kitakachowavutia zaidi watu wengi kwenye club hii itakuwa ni vyumba vya wageni maalumu vya Moet na Chandon, Hennessy na Belvedere. Vyumba hivyo ambavyo vimeunganishwa na huduma ya DSTV, majokofu yenye vinywaji wakati wote, bafu ya ndani kwa ndani, pamoja na muziki.


‘Vyumba hivi ni maalumu kwa kuwakutanisha marafiki wanaofurahia jambo fulani au wateja wanaojadili biashara mbalimbali’ alisisitiza bwana Kadri. Club 327 itakuwa ikifunguliwa siku 5 kwa wiki kutoka Jumanne hadi Jumaipili kuanzia saa mbili usiku na kuendelea. Club 327 pia ina mipango ya kufunguliwa nyakati za mchana kwa watu watakaopendelea kukwepa foleni za katikati ya jiji kupata chakula cha mchana au kufurahia mpira katika luninga nyingi zilizopo kwenye club hiyo.

No comments:

Post a Comment