Jeneza lililobeba mwili wa marehemu Msanii wa Filamu nchini Sadick Juma Kilowoko (SAJUKI) likiwekwa karibu na kaburi tayari kwaajili ya mazishi jijini Dar es Salaam leo. |
Rais Kikwete akiweka mchanga kwenye kaburi la Msanii wa Filamu Sadick Juma Kilowoko wakati wa mazishi yaliyofanyika kwenye makaburi ya Kisutu jijini Dar es Salaam leo. |
Baadhi ya wasanii wakiwa na watu mbalimbali waliohudhuria mazishi ya Msanii Sadick Juma Kilowoko kwenye makaburi ya Kisutu jijini Dar es Salaam leo. |
Rais Kikwete akishuhudia safari ya mwisho ya Msanii wa Filamu nchini Sadick Juma Kilowoko (SAJUKI) wakati wa mazishi hayo yaliyofanyika Kisutu jijini Dar es Salaam. |
Waandishi wa habari wakichukua matukio mbalimbali wakati wa maziko ya Msanii huyo. |
Baadhi ya watu mbalimbali waliohudhuria kwenye msiba huo . |
Mbunge wa Kigoma Kaskazini Zitto Kabwe akihojiwa na waandishi wa habari kwenye makaburi ya Kisutu jijini Dar es Salaam muda mfupi kabla ya mazishi ya msanii Sadick Juma Kilowoko. |
Rais Kikwete akiwasili kwenye makaburi ya Kisutu jijini Dar es Salaam leo kwenye safari ya mwisho ya msanii wa Filamu nchini Sadick Juma Kilowoko (Sajuki). |
Jeneza la mwili wa marehemu Sadick Juma Kilowoko, ukienda kupakizwa kwenye gari. |
Wakisoma dua baada muda mfupi kabla ya kuondoka nyumbani kwake |
No comments:
Post a Comment