Tuzo za watu 2015 zimetolewa Ijumaa hii kwenye hoteli ya Hyatt Regency jijini Dar es Salaam na kushuhudiwa ‘surprises’ za kutosha. Mshindi mkubwa kwenye usiku huo na ambaye amekuwa surprise kwa wengi ni mtangazaji wa TBC FM, D’jaro Arungu aliyeibuka na tuzo mbili.
D’Jaro alikuwa akishindana na Millard Ayo kwenye vipengele hivyo viwili ambaye hata hivyo alishinda pia kipengele cha blog inayopendwa.
“Mtu yeyote aliyekuwa anashindani halafu anaamini anaweza kupata nafasi lazima imshtue,” Millard ameiambia Bongo5.
Hii ni orodha kamili ya washindi
Mtangazaji wa redio anayependwa
D’Jaro Arungu – TBC FM
Kipindi cha redio kinachopendwa
Papaso – TBC FM
Mtangazaji wa runinga anayependwa
Salim Kikeke – BBC Swahili
Kipindi cha runinga kinachopendwa
Mkasi – EATV
Blog/Website inayopendwa
Millardayo.com
Muongozaji wa video anayependwa
Hanscana
Muongozaji wa filamu anayependwa
Vincent ‘Ray’ Kigosi
Muigizaji wa kike wa filamu anayependwa
Wema Sepetu
Muigizaji wa kiume wa filamu anayependwa
Hemedy PHD
Mwanamuziki wa kike anayependwa
Lady Jaydee
Mwanamuziki wa kiume anayependwa
Alikiba
Filamu inayopendwa
Kigodoro
Video ya muziki inayopendwa
Nani kama Mama – Christian Bella f/ Ommy Dimpoz
No comments:
Post a Comment