.

.

.

.

Friday, November 11, 2016

TAASISI ya Kifedha ya Bayport Tanzania Yaadhimisha miaka 10


Wadau mbalimbali wakiwa kwenye hafla hiyo.


Ni furaha tupu katika maadhimisho hayo.


Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Angella Kairuki (kulia), Mjumbe wa Bodi ya Bayport Tanzania, Mama Anna Mkapa (katikati) na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Bayport Tanzania, John Mbaga, wakikata keki katika maadhimisho ya miaka 10 tangu kuanzishwa kwa Bayport Tanzania yaliyofanyika Hyatt Regency Hotel Dar es Salaam juzi.


Mjumbe wa Bodi ya Bayport Tanzania Mama Anna Mkapa (kushoto), na Mwenyekiti wa bodi ya Bayport Tanzania Dkt. Ken Kwaku (katikati) na Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Ali Hapi wakifurahia jambo katika hafla hiyo.



Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Angella Kairuki akihutubia katika hafla ya kutimiza miaka 10 ya Taasisi ya kifedha ya Bayport Tanzania iliyofanyika Hyatt Regency Hotel jijini Dar es Salaam juzi.
Ofisa Mtendaji Mkuu wa Bayport Tanzania, John Mbaga akizungumza kwenye hafla hiyo.
Hafla ikiendelea.
Keki maalumu ya hafla hiyo.
Keki ikiliwa.
Ofisa Mtendaji Mkuu wa Bayport Tanzania, John Mbaga (kushoto), akimlisha keki Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Ali Hapi.



Na Dotto Mwaibale

TAASISI ya Kifedha ya Bayport Tanzania juzi iliadhimisha miaka 10 tangu kuanzishwa kwake na kuelezea mafanikio makubwa iliyopata ndani ya kipindi hicho.

Akizungumza katika hafla hiyo iliyofanyika Hyatt Regency Hotel jijini Dar es Salaam juzi, Ofisa Mtendaji Mkuu wa Bayport Tanzania, John Mbaga alisema ndani ya miaka 10 wameweza kupiga hatua kubwa kwa kuwafikia wananchi wengi.

"Tumepiga hatua kubwa kwa kuwafikia wananchi wengi ambao wamenufaika na huduma zetu" alisema Mbaga.Alisema kupitia taasisi hiyo wananchi wameweza kuanzisha biashara na kujenga nyumba ikiwa ni pamoja na kusomesha watoto.

Mgeni rasmi wa hafla hiyo Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Angella Kairuki alisema Serikali inaipongeza taasisi hiyo kwa huduma za mikopo inayotoa kwa wananchi hivyo kusaidia kuinua pato la taifa na mtu mmoja mmoja.

"Changamoto kubwa iliyopo ambayo mnapaswa kuiangalia ni riba kubwa katika mikopo yenu jaribuni kuliangalia jambo hilo kwa karibu" alisema Kairuki.

No comments:

Post a Comment