CHAMA cha Wananchi (CUF) kimesema hakiko tayari kurejea meza ya mazungumzo kama kilivyoombwa na Chama Cha Mapinduzi (CCM), na badala yake kimetaka pande zinazohusika zisaini makubaliano ili utekelezaji ufanyike.
Hayo yamo katika barua ya Katibu Mkuu wa CUF, Seif Shariff Hamad aliyoiandikia CCM, kujibu barua ya Katibu Mkuu wa chama hicho tawala, Yusuf Makamba kuwaomba kumalizia sehemu iliyobaki katika mazumgumzo yao.
“Ninasikitika kukueleza kwamba utaratibu wa uendeshaji wa siasa za kuwahadaa wananchi kwa kuendesha mazungumzo yasiyo na mwisho si sehemu ya utaratibu wa CUF,” inaeleza barua hiyo ya Hamad.
Maalim Seif Hamad anaongeza kusema: "Kuanzisha upya mazungumzo kupitia Kamati za Makatibu Wakuu haikubaliki kwa upande wa CUF."
Barua hiyo ya Maalim Seif Hamad, yenye kumbukumbu namba CUF/AKM/CCM.11/2008/019 iliyoandikwa Oktoba 8, inawataka CCM kukubali kusainiwa kwa makubaliano ya awali na sio kurejea kwenye mazungumzo ambayo kimsingi yalishakamilika.
No comments:
Post a Comment