.

.

.

.

Friday, October 31, 2008

RAY C KUFUNGA PINGU ZA MAISHA ?

Mwanadada nguli katika uimbaji na kunyonga kiuno chake nchini Tanzania Rehema Chalamila AKA Ray C . anatazamiwa kufunga pingu za maisha na mpenzi wake Lord Eyez wa kundi la Nako2Nako .Wakizungumza kwa kupokezana, wapendanao hao walidai wanaamini kuwa muda umefika wa kufunga pingu za maisha na kuishi kama mke na mume.“Tunamalizia kurekodi nyimbo zetu. Albamu yangu inaitwa ‘Coming of the Real King’ na ya Ray C inaitwa ‘Touch me’. Tukimaliza kurekodi kitakachofuata ni kufunga ndoa tu,” alieleza Lord Eyez.Kauli hiyo ya kuiva kwa mikakati ya kufunga ndoa ilionekana kumfurahisha zaidi Ray C ambaye alikuwa ubavuni mwa Lord Eyez huku akitabasamu na kuchombeza maongezi hayo.“Ni kweli tunatarajia kufunga ndoa hivi karibuni. Muda utakapokaribia tutakuita ili uje kuchukua picha nzuri zaidi za ndoa yetu,” alisema Ray C kwa furaha.Wapenzi hao walibambwa wakipeana maraha ‘chobingo’ usiku wa manane ndani ya Viwanja vya Leaders Club, ambapo siku hiyo kulikuwa na tamasha kubwa la Inter College Bash.

1 comment:

  1. wote wazushi tu huyo dem ana picha za x sasa si anamdanganya mshikaji

    ReplyDelete