.

.

.

.

Friday, October 17, 2008

WARIOBA AKERWA NA UFISADI

WAZIRI Mkuu Mstaafu, Jaji Joseph Warioba, ameonya kuwa wafanyabiashara wanaoonekana kuwa wafadhili wakubwa ndiyo chanzo cha ufisadi huku akisisitiza kuwa kiongozi anayeendekeza kufadhiliwa ni rahisi kuwa kibaraka. Jaji Warioba ambaye amekuwa akikerwa na vitendo vya rushwa nchini na kuvikemea hadharani mara kwa mara, alitoa onyo hilo Dar es Salaam jana wakati akitoa mada kuhusu gharama za kuendesha vyama vya siasa na rushwa katika uchaguzi kwenye kongamano lililoandaliwa na Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa kwa kushirikiana na Taasisi ya Kupambana na Kuzuia Rushwa (TAKUKURU). "Hakuna mfadhili anayetoa fedha zake bila malengo, chama au kiongozi anayetegemea sana wafadhili atakuwa katika hatari ya kujikuta anakuwa kibaraka bila ya kupenda," alionya Jaji Warioba. Alisisitiza kuwa mara nyingi ufisadi katika siasa unatokana na ufadhili. Alitoa mfano kubwa kuwa iwapo vyama vidogo vitashindwa kujiendesha kwa michango ya wanachama wake wachache na wafadhili wa ndani vitakimbilia nje.

No comments:

Post a Comment