.

.

.

.

Wednesday, November 05, 2008

CHID BENZ ------- JE? NDIO MWISHO

Msanii anayebamba zaidi ktk muziki wa Hiphop nchini hivi sasa Chid bez ametangaz akuacha muziki kwa kile alichosema hawezi kuwa mtu wa kuomba msamaha kila siku na watu wakamuelewa.
Chid amezungukwa na utata ktk siku za karibuni baada ya kuripotiwa kumpiga msanii mwenzake Matonya wakati wa tamasha lililofanyika mjini Dodoma.Rapa huyo wa ilala amesema amefikia uamuzi wa kuachana na muziki kutokana na matatizo yanayomwandama ...huku akigoma kueleza undani wa tukio la kumpiga Matonya."Naheshimu kazi yangu, naheshimu mashabiki wangu. Sina ubavu wa kulielezea kila jambo, ila ki-ukweli! ushindani UpO kwa sisi wasanii. Na kwa kazi yetu lazima kuwe na maneno mengi. Siwezi kuomba msamaha kila siku, najua nazidi kuwaudhi mashabiki wangu. Na kiukweli niko juu (hivyo) kila mwenzangu kazini anafurahia ninapopatwa na matatizo kama haya."..."Mashabiki wasini-judge (wasinihukumu) vibaya.....Waamini kuwa hata rais wetu (Jakaya Kikwete) anayependwa sana, toka awe madarakani amekuwa akipata matatizo mengi nafikiri kuliko rais yeyote aliyewahi kuwa madarakani.""Kuna mengi yanatokea katika hiili game lakini nafikiri ya kwanguyamekuwa na bahati ya kusemwa hadharani japo sio makubwa sana ila yanaendana na nilivyo kwa sasa.""Nashukuru kuna watu hawachoki kunipa sapoti...naheshimu leo....Nafikiria Fiesta ya Dar Nov 8 kama nitaruhusiwa kufanya onyesho ndio itakuwa show yangu ya mwisho.Tukio dhidi ya Matonya ni la pili ktk miezi michache baada ya hivi karibuni kufikia kuomba msamaha hadharani kufuatia tukio lililoripotiwa sana la kumpiga Prof Jay.

No comments:

Post a Comment