.

.

.

.

Monday, November 17, 2008

JEETU PATEL AACHIWA KWA DHAMANA


HATIMAYE mfanyabiashara maarufu jijini Dar es Salaam, Jayantkumar Chandubha Patel, maarufu kama Jeetu Patel na ndugu zake wawili wanaokabiliwa na mashtaka ya kughushi na kuiba mabilioni ya fedha katika Akaunti ya Madeni ya Nje (EPA), ndani ya Benki Kuu (BoT), wameachiwa huru kwa dhamana.
Watuhumiwa hiyo wapata dhamana hiyo baada ya kulipa zaidi ya Sh 11.6 bilioni, ili kukidhi masharti ya dhamana hiyo.
Jeetu Patel na wenzake ambao wanakabiliwa na mashitaka manne, wameachiwa huru jana baada ya maombi yao ya dhamana kugonga mwamba kwa zaidi ya wiki moja, kutokana kasoro zilizokuwa zimejitokeza katika nyaraka za wadhamini wao.
Kuachiwa kwa wafanyabishara hao kunafanya idada ya watuhumiwa wa EPA waliachiwa huru kwa dhamana kufikia 12 kati ya 20 waliofikishwa mahakamani.
Awali kabla ya kasoro hizo kujitokeza katika shitakala nne, Jeetu na wenzake ambao mwishoni mwa wiki walitimiza masharti ya dhamana katika mashtaka matatu waliwakirudishwa tena rumande baada ya Mwendesha Mashtaka,Wakili wa Serikali, Fredrick Manyanda kuwawekea pingamizi.
Katika kesi hiyo Namba 1154 inayomshusisha Jeetu na mdogo wake Devendra K.Vinobhai Patel na Amit Nandi kwa pamoja wanadaiwa kuiibia BOT kiasi cha Sh 10.5 bilioni.
Katika masthaka yote manne washitakiwa hao walitakiwa kulipa fedha tasilimu au hati ya mali yenye thamani sawa na nusu ya fedha wanazodaiwa kuziiba na waliwasilisha zaidi ya Sh11.6 bilioni.
Katika hatua nyingine mtuhumiwa mwengine wa wizi huo, Bahati Mahenge ambaye pamoja na wenzake wanne wanadaiwa kuiibia BOT cha zaidi ya Sh2 bilioni kupitia Kampuni yao ya Changanyike Residetial Complex Limited, jana aliachiwa huru baada ya kutimiza masharti ya dhamana.
Watuhumiwa wengine katika kesi hiyo ni wakurugenzi wa kampuni hiyo, Manase Mwakale na mkewe Eddah Mwakale, Davies Kamungu, na Godfrey Moshi. Manase na mkewe waliachiwa huru kwa dhamana mwishoni mwa wiki.
Wakati huo huo, mfanyakazi BoT, Ester Komu jana alijikuta akirudishwa tena mahabusu licha ya kutimiza masharti yote ya dhamana, baada ya Hakimu anayesikiliza kesi yake kutokuwepo mahakamani.
Komu ambaye ni Mkurugenzi Msaidizi katika Idara ya Madeni BoT, amefanikiwa kutimiza masharti ya dhamana baada ya kulipa kiasi cha Sh104 milioni kupitia benki na kuwasilisha risiti mahakamani hapo.

No comments:

Post a Comment