.

.

.

.

Thursday, November 27, 2008

KAGODA! KAGODA! KAGODA ???


WAKATI shinikizo la kutaka kutajwa na kufikishwa mahakamani wamiliki wa Kampuni ya Kagoda Agriculture Limited inayohusishwa kuchota mabilioni ya fedha katika Akaunti ya Malipo ya Madeni ya Nje (EPA) katika Benki Kuu ya Tanzania (BoT) likipamba moto, imedaiwa kuwepo ajenda ya siri ndani ya shinikizo hilo. Pamoja na jitihada za serikali kuhakikisha pesa hizo zinarejeshwa na wale walioshindwa kufanya hivyo, wanafikishwa mahakamani, shinikizo la kutaka Kagoda na wamiliki wake watajwe na kufikishwa mbele ya vyombo vya sheria limeshika kasi ya aina yake. Tayari wanasiasa kadhaa ndani ya chama tawala CCM, kambi ya upinzani na wananchi wamekaririwa wakishinikiza kutajwa na kufikishwa mahakamani kwa wamiliki wa kampuni hiyo mbali ya kuelezwa kuwa imerejesha pesa zote kwa mujibu wa maelekezo ya serikali. Wakati hayo yakiendelea Waziri Mkuu, Mizengo Pinda wiki hii aliwaambia wahariri wa vyombo vya habari kwamba mlipuko wa shinikizo kutoka pande mbalimbali za jamii unaoendelea sasa utasababisha kujulikana ukweli wote unaoihusu Kampuni ya Kagoda.

No comments:

Post a Comment