.

.

.

.

Thursday, November 13, 2008

TANGAZO CCM TAWI LA LONDON

KUSITISHWA KWA UCHAGUZI WA WAJUMBE KUMI NA TANO (15) WA HALMASHAURI KUU - NGAZI YA TAWI LA CCM LONDON (UK)

Wanachama wa Chama Cha Mapinduzi, Tawi la London (Uingereza)Nachukua nafasi hii kuwafahamisha kuwa uchaguzi wa viongozi wa kudumu wa Wajumbe Kumi na Tano (15) wa Halmashauri Kuu - ngazi ya Tawi la CCM London (UK), kama ulivyotangazwa awali kuwa ungefanyika pamoja Mkutano Mkuu wa Tawi huko London, Jumapili tarehe 16 Novemba 2008 umesitishwa (postponed), mpaka hapo tarehe mpya itakapotolewa.

Hii ni kutokana na sababu zilizoshindikana kupatiwa ufumbuzi wa haraka. Tutawajulisha mapema kuhusu tarehe mpya. Tunaomba radhi kwa usumbufu uliotokea, na pia tunashukuru kwa ushirikiano wenu. Kidumu Chama Cha Mapinduzi

No comments:

Post a Comment