.

.

.

.

Saturday, December 06, 2008

JAHAZI MODERN TAARABU KUKWEA PIPA IJUMAA


Jahazi Modern Taarab kwenda Uingereza Ijumaa
Kundi zima la Jahazi Modern taarab, linaondoka nchini kuja uingereza siku ya Ijumaa asubuhi na Ndege ya "British Airways" tayari kwa shoo yake itakayofanyika siku ya Jumamosi katika ukumbi wa Silverspoon, uliopo pembeni ya uwanja wa Wembley.

Akizungumza na waandishi wa habari jana, kiongozi wa kundi hilo, Mzee Yusuph, alisema kundi zima linaondoka na wanatarajia kurudi Dar es salaam tarehe 24 tayari kwa safari ya mkoani Tanga siku ya mkesha wa sikukuu ya Krismass.

Mzee Yusuph alisema hadi sasa wanafahamu kuwa watafanya onesho moja, hadi hapo wenyeji wao kampuni ya Jambo Publication Limited itakapotoa mwongozo wa shoo nyingine,lakini hadi sasa tunachojua kuwakuwa na shoo hiyo ya kusheherekea sikukuu ya miaka 47 ya uhuru wa Tanzania.

"Tunatarajia kutoa burudani safi kwa mashabiki wetu wa London na vitongoji vyake, tunakwenda kuwapata 'two in one' yaanikusheherekea sikukuu ya Idd El Hajji na sikukuu ya Uhuru, lakini pia na sisi tutawapa zawadi ya wimbo wetu wa Two in One, " alisema Mzee Yusuph.

Mratibu wa kampuni ya Jambo Publications inayodhamini safari ya kundi hilo, Juma Mabakila alisema maandalizi yote ya onesho hilo yamekamilika na iliyobaki siku yenyewe kuwadia na kuwataka mashabiki kuwahi mapema kwani ukumbi mwisho kuchukua watu 600 tu.

"Tumepewa onyo na wamiliki wa ukumbi kuwa hakutakuwa na watu wa ziada baada ya kufikia watu 600, hiyo aliwataka wale wanaotoka mbali kupiga simu namba 02083265606-7 na kuorodhesha jina ili hata ukichelewa jina lako litakuwa mlangoni ili kuepuka usumbufu,"alisema Mabakila.

Alisema mipango ipo mbioni kuhakikisha kuwa kuwe na shoo nyingine mbali ya hii ya London na kama kuwatakuwa na shoo hizo basi zitatangazwa siku ya Jumamosi ili kutoa nafasi kwa watu wengine watakaokosa nafasi kuwaona Jahazi.

No comments:

Post a Comment