MICHUANO ya Kombe la Tusker itaanza kutimua vumbi Desemba 15, lakini mabingwa watetezi Yanga wataingia uwanjani kuonyeshana kazi na URA ya Uganda siku mbili baadaye na watani zao Simba wakisubiri siku moja zaidi kucheza na Prisons ya Mbeya.
Kwa mujibu wa ratiba iliyotolewa na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Yanga imepangwa Kundi A pamoja na URA na Mtibwa huku Simba ikiwa Kundi B na wababe wao Tusker FC ya Kenya na Prisons.
Katika mashindano hayo bingwa atajinyakulia Shilingi mil.40, na katika siku ya ufunguzi kutakuwa na mechi ya moja itayozikutanisha Mtibwa na URA huku Tusker na Prisons zikicheza siku inayofuata.
Yanga imeingia kwenye michuano hiyo kwa kujiamini kuwa wanaweza kutetea ubingwa wake kutokana na kusheheni kikosi imara ambacho kina wachezaji wengi wa kimataifa na pia wanaongoza Ligi Kuu ya Tanzania Bara kwa pointi 30.
Simba nayo ikiwa na historia ya kutwaa kombe hilo mara nyingi zaidi kuliko timu yoyote imepania kurirudisha taji hilo mkononi mwake msimu huu baada ya mwaka jana kujitoa kwa madai wadhamini walitoa fedha kiduchu.
" Tuliwaachia tu Yanga, wenyewe tumerudi sasa baada ya wadhamini kuongeza fedha tunarejea kwa kasi na kulirudisha kombe letu," alisema Mwina Kaduguda wakati akipokea vifaa jana kutoka kwa wadhamini wa michuano hiyo bia ya Tusker.
Katibu Mkuu wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Fredirick Mwakalebela alisema Yanga na Simba imebidi zisubiri hadi Desemba 17 na 18 kutokana na wachezaji wake wengi kuwa timu ya Taifa Stars ambayo inaondoka wiki ijayo kucheza mchezo wa marudiano dhidi ya Sudan.
"Tutajitahidi kuhakikisha mashindano haya yanafanyika kwa mafanikio na yawe mashindano bora ya mfano wa kuigwa na kuiletea sifa nchi, wadhamini na yawe changamoto kwa timu ambazo hazishiriki.
"Ratiba hii imeangalia mambo mengi ikiwemo Simba na Yanga ambazo zina wachezaji wengi timu ya taifa na ndio maana mechi zao zinachezwa siku mbili baada ya kuanza kwa mashindano kwani nina uhakika Stars itakuwa imerejea kutoka Sudan na wachezaji watakuwa wamepumzika kwa siku mbili na kurudi katika klabu zao na kuendelea na mashindano ya Tusker," alisema Mwakalebela.
Mwakalebela aliongeza kuwa mashindano hayo pia hayataathiri kambi ya Taifa Stars inayojiandaa kwa ajili ya michuano ya Challenge itakayoanza Desemba 31, Uganda.
" Kambi itaanza Desemba 27, lakini
No comments:
Post a Comment