.

.

.

.

Monday, December 08, 2008

MEET AND GREET PARTY BONGO KEMPSKI HOTEL

Pichani pili kushoto ni Eve E akizungumza na waandishi wa habari leo jioni ( hawapo pichani) ndani ya hoteli ya Kilimanjaro Kempisk akizungumzia onesho lao linalofanyika usiku huu kwenye viwanja vya Gymkana Club.Shoto ni mratibu wa shoo hiyo kutoka Prime Time Promotions/Clouds Fm,na wanaofuata kutoka Eve ni wawakilishi kutoka kampuni ya TCC ambayo ndio wadhamini wakuu wa onesho hili. Eve E ameweka wazi kuwa yeye yuko safi kabisa kwa shoo ya usiku huu na yoyote ambaye tayari amekwishakata tiketi yake basi ajue wazi atajiachia vya kutosha.Mbali ya wasanii hao pia watakuwepo wasanii wengine wanaotamba kwa sasa kutoka nchini Nigeria P-Square pamoja na wasanii wa hapa nyumbani akiwemo Ay na Mwana-FA ambao watafanya utambulisho wa albamu yao iitwayo Habari ndiyo Hiyo.
Big Joe Mkurugenzi wa PTP na Cloudsfm (pili shoto) ,mkewe na shemeji yake katika picha ya pamoja na Fat Joe

Eve akijiachia kinoma


Madjei maarufu wa cloudsfm pamoja na EVE




Pozi la kina dada waliokuwepo kumpa shavu kimwana Eve




palikuwa hapatoshi jinsi watu walivyvojirusha

Picha kwa hisani ya MICHUZIJR.


No comments:

Post a Comment