Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe, amesema ana ushahidi kuwa, Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Lawrence Masha ndiye aliyepeleka hoja ya kumhujumu Mwenyekiti wa IPP, Reginald Mengi katika vikao vya juu na kwamba taarifa hizo alithibitisha kuzipata jana. Akiongea jana, Zitto alisema waziri huyo, kwa taarifa alizonazo za kuaminika, alitoa hoja kuwa vyombo vya habari vya IPP vimekuwa mstari wa mbele kupiga vita ufisadi na hii inailetea matatizo serikali. Hivyo, aliomba serikali ipange mikakati ya kumfilisi Mengi, kitendo ambacho kitasababisha kudhoofishwa kwa vyombo vyake vya habari ambavyo vitashindwa kuendelea kuupinga ufisadi. Zitto alisema yeye hana sababu ya kumtetea Mengi ila hawezi kunyamaza kuona Mtanzania anayeipenda nchi yake na kulazimika kupinga ufisadi anafanyiwa hujuma..
.
Sunday, December 07, 2008
ZITTO APASUA JIPU
Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe, amesema ana ushahidi kuwa, Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Lawrence Masha ndiye aliyepeleka hoja ya kumhujumu Mwenyekiti wa IPP, Reginald Mengi katika vikao vya juu na kwamba taarifa hizo alithibitisha kuzipata jana. Akiongea jana, Zitto alisema waziri huyo, kwa taarifa alizonazo za kuaminika, alitoa hoja kuwa vyombo vya habari vya IPP vimekuwa mstari wa mbele kupiga vita ufisadi na hii inailetea matatizo serikali. Hivyo, aliomba serikali ipange mikakati ya kumfilisi Mengi, kitendo ambacho kitasababisha kudhoofishwa kwa vyombo vyake vya habari ambavyo vitashindwa kuendelea kuupinga ufisadi. Zitto alisema yeye hana sababu ya kumtetea Mengi ila hawezi kunyamaza kuona Mtanzania anayeipenda nchi yake na kulazimika kupinga ufisadi anafanyiwa hujuma.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment