.

.

.

.

Monday, January 19, 2009

SOO LINGINGINE KWA RAIS MSTAAFU


RAIS wa serikali ya awamu ya tatu, Benjamin Mkapa, ambaye amekuwa akisakamwa kwa tuhuma za matumizi mabaya ya ofisi, huku akitakiwa kuvuliwa kinga na kupandishwa kizimbani, sasa anakabiliwa na tuhuma nyingine nzito; anatakiwa afikishwe Mahakama ya The Hague baada ya Wapemba kuuawa Januari 27, 2001.
Mauaji ya Wapemba hao yalitokea mara baada ya kutangazwa kwa matokeo ya urais wa Zanzibar wakati Amaan Abeid Karume alipotangazwa mshindi na kusababisha wapinzani kuandamana kupinga ushindi huo. Serikali inasema ni watu wasiozidi 27 ambao waliuawa, lakini wapinzani wanasema ni zaidi ya 100.
Na wazee wa Pemba walioshiriki kuandaa barua ya kuuomba Umoja wa Mataifa uwasaidie kupatikana kwa serikali huru ya kisiwa hicho, ndio walioibua hoja hiyo wakisema wanakusudia kumfikisha rais wa awamu ya tatu, Benjamin Mkapa Mahakama ya The Hague kutokana na mauaji waliyoyaita ya kikatili ya Wapemba yaliyotokea Januari 27 mwaka 2001.
Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, katibu mtendaji wa wazee hao, Hamad Ali Musa, alisema tayari walishafikisha suala hilo kwenye ofisi za Umoja wa Mataifa kwani mauaji hayo yalitokea wakati viongozi hao wakiwa madarakani.

No comments:

Post a Comment