.

.

.

.

Friday, March 20, 2009

BAADA YA ALBINO SASA NI KUBAKA VITOTO

VITENDO vya ubakaji vimeanza kushamiri mkoani Iringa, huku matukio ya hivi karibuni yakionesha wanaokumbwa na sakata hilo wakiwa ni watoto wa kike wenye umri chini ya miaka sita.

Katika matukio mawili yaliyotokea ndani ya wiki tatu, mtoto mmoja amekufa baada ya kufanyiwa unyama huo huku mwingine akiendelea kutibiwa katika hospitali ya Mkoa wa Iringa. Tukio lililopelekea mmoja wa watoto hao kufa lilitokea majuzi, baada ya mtoto huyo (jina linahifadhiwa) kubakwa na watu wasiojulikana hadi mauti yake yalipomfika na hatimaye kutupwa kwenye bonde dogo la mlima Tagamenda uliopo mita 600 kutoka stendi ndogo ya mabasi ya mikoani ya Ipogolo ya Iringa mjini.

Polisi waliokuwepo kwenye eneo hilo walifanikiwa kuutoa mwili wa mtoto huyo mwenye miaka mitano kutoka katika bonde hilo lenye miti mingi yenye miba akiwa hana nguo na amelowa damu sehemu zake za siri, huku umati mkubwa wa watu waliokuwepo wakiangua kilio kwa uchungu.

No comments:

Post a Comment