.

.

.

.

Monday, March 30, 2009

TAIKUNI SOMAIYA ATOROKA MAKACHERO

BILIONEA Ketan Somaia, anaetafutwa nchini Tanzania kwa tuhuma za utapeli, ameponyoka wakati akiwa chini ya mikono ya makachero wa Kenya.
Hatua hiyo imekuja wakati akiwa mbioni kumaliza kifungo chake na kisha kurejeshwa nchini Tanzania, kujibu tuhuma za utapeli dhidi ya mfanyabiashara Vincet Laswai na ufisadi wa makampuni yake ya Somaia Group.
Duru za kuaminika kutoka Idara ya Polisi wa Kimataifa nchini Tanzania (Interpol) na ambazo zimethibitishwa na Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI) Kamishna Robert Manumba, zilisema Somai anasadikiwa kukimbimbilia India.


Kwa mujibu wa taarifa hizo, Somaia ambaye alikuwa maarufu nchini akiwa na viwanda chini ya mwavuli wa Somaia Group, alitoroka baada ya kupata dhamana katika rufaa yake katika MahakamaKuu ya Kenya.
Duru hizo zilisema baada ya kukata rufaa na kutoka nje, Somia alitoroka na hadi sasa makachero wa Kenya hawajui aliko.
Kwa mujibu wa duru hizo, baada ya kuhukumiwa kifungo cha miaka mitatu, raia huyo wa India, alikata rufaa iliyotengea adhabu hiyo.
Hata hivyo, wakati mchakato wa kisheria ukiendelea, Somaia alipata upenyo wa kuwaponyoka makachero wa Kenya na kukimbilia India.
Kwa mujibu wa duru hizo, taarifa hizo zimeishitua na kuchukiza Jeshi la Polisi nchini ambalo ndilo lilisaidia kukamatwa kwa mtuhumiwa, alipokuwa akijandaa kutoroka Afrika, kupitia uwanja wa ndege wa Jomo Kenyatta.
Akizungumzia taarifa hizo mishoni mwa wiki iliyopita Mkurugenzi Manumba alikiri kuhusu Interpol ya Tanzania kupata taarifa hizo.
Kwa mujibu wa DCI Manumba, Polisi wa Tanzania kwa kushirikiana na Interpol ya India na Kenya, wanaendelea kumsaka mtuhumiwa huyo.

No comments:

Post a Comment