Mtuhumiwa anayeongoza kwa kuwa na kesi nyingi za ufisadi wa mabilioni ya fedha katika akaunti ya malipo ya madeni ya nje (EPA) katika Benki Kuu ya Tanzania (BOT) Jeetu Patel (kulia) akifuatilia kwa karibu kesi ya kina mramba kabla ya yeye kuitwa kizimbani leo.
Watuhumiwa katika kesi hiyo kutoka kulia ni Daniel Yona, Basil Mramba na Grey Mgonnja wakiwa ndani ya Mahakama ya Kisutu wakitafakari kabla ya kupanda kizimbani.Hatimaye kesi ya ufisadi na matumizi mabaya ya ofisi inayowakabili aliyekuwa Waziri wa Fedha, Basil Pesambili Mramba , aliyekuwa Waziri wa Nishati na Madini, Daniel Yona na aliyekuwa Katibu Mkuu Wizara ya Fedha Grey Mgonja imeanza kusikilizwa leo katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Jijini Dar es Salaam mbele ya Hakimu wa Mahakama hiyo Hezron Mwankenja ambapo jumla ya Mashahidi 13 wanatarajiwa kuitwa na upande wa Jamuhuri. Kesi hiyo imeahirishwa hadi Mei 18 mwaka huu.
No comments:
Post a Comment