.

.

.

.

Monday, April 27, 2009

YNONNE CHAKACHAKA ABUBUJIKWA MACHOZI MTWARA

MWANAMUZIKI wa Afrika Kusini, Yvonne Chakachaka ijumaa iliopita alibubujikwa na machozi baada ya kusikia kuwa mtoto aliyekuwa amelazwa kwa malaria amefariki dunia na mama yake kuondoka na maiti mgongoni.

Yvonne ambaye pia ni Balozi wa Malaria duniani alikuwa akigawa vyandarua vyenye dawa katika wodi namba tano ya hospitali ya Mkoa wa Mtwara, Lugula alipokuwa amelazwa mtoto huyo.
Alipofika wodini hapo, aliambiwa kuwa alikuwapo mgonjwa huyo, lakini alifariki dunia jana na mama yake akalazimika kuubeba mwili wa marehemu mgongoni kutokana na kukosa usafiri, ndipo mwanamuziki huyo alishindwa kuzuia machozi.
“Najua wengi mmeshangaa nilivyolia, lakini kama mzazi imeniuma, kwa kuwa siamini kama kunaweza kuwa na tukio kama hilo katika bara letu la Afrika,” alisema.

Alisema hiyo ilikuwa siku mbaya maishani kwake na hawezi kuondokana na kumbukumbu ya tukio hilo.
“Nimeamua kununua gari moja ambalo litakuwa linatumika maalum kwa ajili ya kina mama na watoto wanaosumbuliwa na ugonjwa huu sugu hapa nchini.”

Alisema kuwa kwa sasa anaangalia uwezekano wa kuja kuishi nchini na kama ikiwezekana iwe Mtwara, ili aweze kusaidiana na akinamama ambao wanapata matatizo ya watoto na uzazi. “Sioni sababu ya sehemu kama hii nzuri kuwa na matatizo, mimi nimeipenda Mtwara, nimetembelea baadhi ya mikoa Tanzania, lakini naona nchi hii ni ya kuwa makazi yangu ya baadaye,” alisema.

Chakachaka ambaye aliwasiri wiki iliopita kwa ajili ya kushuhudia maadhimisho ya siku ya Malaria duniani alitembelea Hospitali ya Ligula na baadaye kufanya onyesho katika viwanja vya mashujaa na kuhutubia wananchi.

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda aliyekuwa mgeni rasmi, alisema kuwa mikoa ya kanda ya ziwa ndio imekuwa ikiongoza nchini kwa kuwa na asilimia 34 ya maambukizo ya malaria ikifuatiwa na mikoa ya kusini asilimia 30 na mikoa ya magharibi asilimia 21 wakati mikoa mingine ni asilimia 14.

No comments:

Post a Comment