.

.

.

.

Wednesday, June 17, 2009

JE INAWEZEKANA TANZANIA ???

Viongozi wa Kenya wameamua kuuza magari yote ya kifahari na fedha itakayopatikana itatumika kwa shughuli mbalimbali za kuwasaidia masikini ikiwemo wale walioathirika na kuhama kutokana na mapigano mara baada ya uchaguzi mkuu wa mwaka jana. Badala ya magari ya kifahari sasa viongozi wa nchi hiyo watapatiwa magari ya kawaida kama vile Volkswagen, Toyota Corolla, Celica, Cresta na mengine kama haya. Mapinduzi haya inaelekea yanaletwa na mtoto wa Familia ya Kitajiri na wa Rais wa kwanza wa Kenya ambaye sasa kajifunza kuwa yeye kuwa tajiri na kuishi kifahari wakati Wakenya wengi ni masikini wa kutupwa ni sawa na kukufuru.

Wachunguzi wa kisiasa wanajiuliza hivi nchi ambayo ingelifanya jambo hili ni Kenya au Tanzania. Majibu ya baadhi yao ni kwamba viongozi wengi wa kitanzania wanatokea familia za Kimasikni na wakiukwaa utajiri kwa njia za halali au wizi inakuwa kama vile kipofu kauona mwezi. Wale wanaotokea familia za Kitajiri hawajawahi kufunzwa lolote na wazazi wao kuhusu maana na sababu ya kuwepo hapa duniani. Na wanachukulia kwamba kuwa na magari ya kifahari, majumba makubwa na kutapanya pesa katika anasa binafsi ni haki yao.
SOURCE : JAMIIFORUMS

No comments:

Post a Comment