.

.

.

.

Friday, June 19, 2009

KASEJA AREJEA SIMBA


KIPA wa zamani wa klabu ya Yanga, Juma Kaseja amemwaga wino katika klabu yake ya zamani, Simba jana.
Habari zilizoifikia Mwananchi jana zimesema kuwa usajili huo umefanikishwa na kamati ya usajili wa klabu hiyo na mfadhiri mmoja ambaye jina lake linahifadhiwa.
Chanzo chetu kilisema kuwa kufanikiwa kwa zoezi hilo ni faraja kubwa kwa wapenzi na wanachama wa klabu ya Simba baada ya kipa huyo kuihama mwaka jana na kujiunga na wapinzani wao wa jadi kwa mkataba mnono.
Kufanikishwa kwa zoezi hilo kumeondoa minongĂ­ono mingi iliyokuwepo na hasa baada ya kipa huyo kubainika kuwa alikuwa bado hajasaini fomu za usajili.
Kuna kipindi ilisemekana atajiunga na African Lyon, hata hivyo uongozi wa timu hiyo kupitia mmiliki wake, Mohammed Dewji ulikanusha. Baadaye ikavumishwa kuwa alikuwa na mpango wa kujiunga na Azam FC, nako kukawa kimya.
SOURCE :Mwananchi

No comments:

Post a Comment