.

.

.

.

Sunday, June 14, 2009

MIKOA MINANE KUKOSA UMEME

SHIRIKA la umeme nchini(Tanesco), limeeleza kuwa mikoa ya Mwanza, Shinyanga, Tanga, Arusha, Kilimanjaro, Singida, Mara na Tabora itaingia kwenye mgawo wa umeme kuanzia leo hadi Julai 13.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari juzi na Meneja Mawasiliano wa shirika hilo, Badra Masoud, ameeleza kuwa shirika hilo, litasimamisha shughuli za ufuaji wa umeme wa mtambo wake wa maporomoko wa New Pangani, kwa ajili ya marekebisho makubwa.
Kutokana na marekebisho hayo, Masoud ameeleza kuwa umeme utapungua kwa megawati 68 katika gridi ya taifa, hivyo mikoa hiyo itaingia katika mgawo wa umeme kwa takriban saa nne.
Masoud alieleza kuwa, kutokana na sababu hiyo nishati ya umeme inayopelekwa Kaskazini Magharibi mwa gridi ya taifa, italazimika kupitia katika njia kuu ya umeme Mtera mkoani Dodoma, ambayo iko katika hali ya kuzidiwa katika usafirishaji wa nishati ya umeme.
Mtambo huo, utazimwa kuanzia leo hadi Julai 13 mwaka huu.

No comments:

Post a Comment