.

.

.

.

Tuesday, June 16, 2009

MISS VYUO VIKUU KUFANYIKA JULAI 3

WAREMBO 15 wamejitokeza kushiriki katika shindano la kumsaka mrembo wa Vyuo Vikuu lililopangwa kufanyika Julai 3 katika ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam.
Akizungumza na waandishi wa habari jana, kwenye mkutano uliofanyika katika ukumbi wa Hadees , Mratibu wa shindano hilo, Manka Mushi, alisema warembo hao walianza mazoezi jana katika ukumbi wa Club Bilicanas.
Mratibu huyo alisema kutokana na shindano hilo kushirikisha idadi kubwa ya wanafunzi kutoka katika vyuo mbalimbali vya jijini Dar es Salaam, ambao kwa sasa wako kwenye mitihani, hivyo watajiandaa na shindano hilo kwa wiki moja kabla ya shindano hilo.
Washiriki hao watakuwa chini ya aliyekuwa Miss Tanzania namba tatu, Pendo Laizer, ambaye pia alikuwa Miss Vyuo Vikuu wa mwaka jana.
Manka alivitaja vyuo vilivyotoa washiriki ni Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Chuo cha Uandishi wa Habari Tanzania (TSJ), Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM), Chuo cha Ustawi wa Jamii (ISW), Chuo cha Biashara (CBE) na Chuo cha Jakaya Kikwete kilichopo Kurasini.


Wadhamini wa shindano hilo ni Vodacom Tanzania, TDL kupitia mvinyo wa Overmeer, Ben Expedition Tours, Air Tanzania, Ndege Insurance Co, Tesco Furniture, Clouds FM kupitia kipindi cha Leo Tena na Perfect Solutions.
Wengine ni Global Publishers, Club Bilicanas, Rosella Saloon, Full Shangwe Blogsport, City Stars Boutique, Dollwood, Valley Spring, Zizzou Fashion, Carpuany Design, Hartman Production na Kampuni ya ulinzi ya Aurora.

No comments:

Post a Comment