.

.

.

.

Monday, July 20, 2009

JIBWA LA AJABU BONGO
Jibwa moja linalodaiwa kuwa na matendo ya ajabu kiasi cha baadhi ya watu kuliita mbwa - mtu limezuka ghafla na kuibua hofu ya aina yake kwa wakazi wa maeneo ya Goba Jijini baada ya kutafuna kuku kibao na kujeruhi watu kadhaa, wakiwemo wanne ambao wamefikishwa hosputalini.
Jibwa hilo, ambalo baadhi ya watu wanadai ni jeusi na lenye mimacho mikubwa ya kung'aa, limeshamjeruhi mama mmoja aitwaye Bibi Tina, mtoto aitwaye Hussein, mwanamama Theresa Robert na Mzee Gideon Mkwawi.
Mjumbe mmojawapo wa Serikali ya Mtaa wa Goba, Bw. Laurent Joseph Mtego, amesema hofu imekuwa kubwa kwa wananachi wa eneo lao hasa baada ya watu kujeruhiwa na watatu kuhamishwa toka katika Zahanati ya Goba na kupelekwa katika Hospitali ya Magomeni, Jijini.
"Kwakweli hali imekuwa ya mashaka, hasa nyakati za usiku... ila tumeshaanza mikakati ya kukabiliana na tishio hili, ikiwa ni pamoja na kuwasihi watu wanaong'atwa kuwahi hospitalini," amesema Bw. Mtego.
Aidha, akasema kuwa yeye na viongozi wenzie hawaamini kuwa tukio la jibwa hilo linahusiana na ushirikina.
"Tunahofia kuwa isije ikawa ni kichaa cha mbwa... ndio maana kuna hatua kadhaa ambazo naamini viongozi wa juu wa mtaa wameshaanza kuchukua ili kuwasiliana na wataalam wa manispaa... na hadi sasa, baadhi ya mbwa waliong'atwa na hilo jibwa tumeshawaua kwa marungu kwa kuhofia kuwa isije ikawa wamepata kichaa cha mbwa," akasema Bw. Mtego.

No comments:

Post a Comment