.

.

.

.

Thursday, November 24, 2011

AJALI MBAYA SANA YATOKEA D'SALAAM

Wakazi wa Jiji Dar es salaam wakiangalia gari dogo lililoharibiwa vibaya baada ya kugongwa na lori jana
Polisi akiangalia moja ya magari mawili yaliyopata ajali mbaya kwa kugongwa na lori la mafuta T 264 BUC Barabara ya Mandela, Dar es salaam jana.
Askari wa Usalama Barabarani akiwa amebeba Kichwa cha mtu aliyefariki baada ya kugongwa na lori jana maeneo ya Riverside Ubungo Jijini Dar es salaam.
WATU wawili wamekufa na wengine wanne kujeruhiwa vibaya baada ajali mbaya iliyotokea jana saa saba mchana katika eneo la
Ubungo Riverside, Jijini Dar es Salaam.

Ajali hiyo ilihusisha lori la mafuta lenye namba za usajili T 269 BRQ na tela lenye namba T 264 BUC, ambalo lilikuwa likitoka Ubungo kwenda Buguruni, kuhama upande wa pili wa barabara, kugonga magari saba madogo na kuanguka.

Magari yaliyogongwa ni T 112 BTT aina ya Saloon, T 133 ADC Toyota chesar, T 918 BHC Toyota Colola, T 969 AVM Canter, T 302 AVC Pickup na T 501 BJH aina ya Noah ambayo yalikuwa yakitokea Buguruni kuelekea Ubungo.

Akizungumza na Majira, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi Kinondoni, Charles Kenyela, aliwataja waliokufa kuwa ni Bw. Venoni Sebastiani(38) mkazi wa Tabata Kinyelezi, ambaye alikanyagwa na lori hilo wakati akivuka barabara.

Kamanda Kenyela alisema, ajali hiyo pia ilisababisha kifo cha mwanamke mjamzito ambaye jina lake halijafahamika hadi sasa.

“Huyu mwanamke alikuwa akivuka barabara ndipo alipogongwa na lori, kichwa chake kilikatika na kutenganishwa kiwiliwili, rereva wa lori alikuwa akikwepa daladala iliyokuwa ikitoka kituoni wakati akiwa mwendo kasi ndio lihamaha barabara,” alisema.


Aliongeza kuwa, mama huyo alipondwa na kusagika pamoja na kichanga kilichokuwa tumboni.

Aliwataja majeruhi wa ajali hiyo kuwa ni Bw. Musa Charles (35), mkazi wa Kinondoni ambaye alikatika miguu yote miwili na kulazwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili na Bw. Yahaya Makame Mhadhili wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.

Wengine ni Bw. Abasi Julius (24), mkazi wa mkazi wa Vingunguti na Bw. Prospa Mwakitaluma (34), mkazi wa Ubungo Changanyikeni ambao wote wamelazwa Hosptitali ya Amana.

Akizungumza na waandishi wa habari katika eneo la tukio, dereva wa gari namba T 302 AVC ambaye alinusurika katika ajali hiyo Bw. Said Sadick, alisema chanzo cha ajali hiyo ni mwendo kasi wa lori ambalo lilikuwa likikwepa daladala.

“Kama angeligonga daladala hilo, angesababisha vifo vya watu wengi zaidi ndio maana alichukua uamuzi wa kulikwepa, daladala husika iliondoka bila kukamatwa,” alisema.

Kwa upande wake, Dereva wa gari namba T501 BJH, ambaye alijitambulisha kwa jina moja Bi. Anna, alisema chanzo cha ajali hiyo ni dereva wa daladala ambaye alikuwa akitoka kituoni bila kuchukua tahadhari

2 comments:

  1. Ajali kwa kusema ukweli zimezidi na zinatisha mimi hii nchi ninayo kaa haswa mji ninao kaa sijawahi ona ajali tangu nifike na sasa ni mwaka na nusu,ila sasa kila nikiangalia newz humu nakuta ajali jamani tujifunze kufata sheria mwendo kasi sio faida.Inauma sana kupoteza ndugu kila siku tena kwa ajali za kutisha.

    ReplyDelete
  2. Daladala zina sababisha ajali nyingi.. Serikali fungiya DalaDala moja kwa moja, weka usafiri wa serikali mabasi ambayo yaondoke kwa wakati na kurejea kwa wakati kama nchi nyengine zenye kusalimisha maisha ya wananchi wao.

    ReplyDelete