.
.
Friday, July 24, 2009
MZEE MORRIS NA NGOMA ZAKE KUMI
Namzungumzia Mzee Morris Nyunyusa. Mkongwe aliyekuwa mahiri katika upigaji wa zaidi ya ngoma kumi japo alikuwa maarufu kwa “ngoma zake kumi.” Namkumbuka sana mzee huyu japo wakati akifanya vitu vyake sikubahatika kumwona. Hata hivyo nilimwona kupitia ngoma zake zilizosikika na zinazoendelea kusikika katika redio Tanzania na sasa TBC taifa.Umahiri wa mzee Morris ulivuma sana miaka hiyo na kufanya apate mialiko mingi ndani na nje ya nchi. Nakumbuka [kwa mujibu wa vyombo vya habari wakati huo] mojawapo ya nchi aliyokwenda mzee Morris ni Japan. Aliyenikumbusha kuhusu mzee Morris ni mgeni mmojawapo katika blogu yangu. Sasa naahidi panapo majaaliwa nitawaletea habari kuhusu maisha ya mzee Morris Nyunyusa muda mfupi ujao, cha msingi tuombe majaaliwa ya mwenyezi mungu. Wageni wangu mtamfahamu mzee yule nje ndani na mazingira ambayo familia yake inaishi hivi sasa. Je, umaarufu wa baba yao unawawezesha kuishi maisha bora au kasahaulika kama walivyosahaulika mashujaa wenzie lukuki?Pamoja na maneno mengi ambayo tunaweza kusema kumuhusu mzee Morris lakini neno moja halitakuwa na hata chembe ya uongo. Neno hilo ni kwamba ngoma za mzee Morris bado zingali hai.Mwisho wa mwanzo…..
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment